Yanga Yaweka Rekodi Mpya

YANGA imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuvunja rekodi yake ya mabao 44, ambayo walifunga msimu uliopita Msimu uliopita Yanga ilimaliza kwenye nafasi ya tatu, katika msimamo huo, huku Simba ikitwaa ubingwa, ambapo timu zote zilicheza mechi 30 za ligi.

 

Yanga imevunja rekodi hiyo, baada ya mechi 27 za msimu huu kufunga mabao 45 ikiwa imevunja ile ya mabao 44 waliyoweka msimu wa 2017/18. Timu hiyo imecheza mechi 27, msimu huu na kushinda mechi 21 na kati ya hizo imepoteza mbili na kutoa sare nne, ikikusanya pointi 67.

 

Yanga imesaliwa na mechi 11 ili kukamilisha mzunguko wa pili ambapo inatakiwa kucheza jumla ya mechi 38 msimu huu. Msimu uliopita, ilimaliza kwa kufunga mabao 44 na kukusanya pointi 58, huku ikiruhusu wapinzani wake kuingia wavuni mara 23.

 

Kwa maana hiyo Yanga imevunja rekodi yake ya msimu uliopita. Mbali na mabao ya msimu uliopita mpaka ligi inamalizika, Yanga ilikuwa imeshinda mechi 14, pekee lakini sasa timu hiyo imeshinda mechi 21 kati ya 27 walizocheza.

 

Hii ina maana kuwa Yanga wana nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri kuliko msimu huo kwa kuwa bado hata hawajafikia mechi 30 walizocheza msimu mzima.

Toa comment