The House of Favourite Newspapers

Yanga Zenji Watamba Kuimaliza Simba Leo

0

MASHABIKI wa Yanga wamesema kitakachotokea leo Jumamosi Uwanja wa Mkapa, Dar, kitaweka historia kwa timu ya Simba, hivyo wale ambao wana mioyo dhaifu ni vyema watulie majumbani mwao.

 

Simba watakuwa wenyeji wa Yanga leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, mashabiki sugu wa Yanga, Abdullah Kombo kutokea Mtaa wa Amani na Ali Mohammed kutokea Mtaa wa Tomondo hapa Mkoa wa Mjini Unguja, walisema kikosi chao kesho kitaweka historia jijini Dar es Salaam hata nje ya Dar es Salaam kwani uwezo mkubwa wa kushinda mchezo huo wanao.

 

Walisema mpira ni dakika 90 ila kwao wao dakika 90 zitamalizika wakiwa washindi, hivyo ikiwa kuna shabiki wa Simba mwenye presha au tatizo la moyo, bora abakie nyumbani kwake ili kuepuka mshtuko wa mabao ya uwanjani.

 

Kwa upande wa shabiki wa Simba, Ally Suba kutokea Mtaa wa Mtoni Kidatu, alisema hawatishwi kwa maneno au kwa majina makubwa, hivyo wao hawana hofu na mchezo wao dhidi ya mahasimu wao.

 

“Niseme tu hatuna hofu na hii mechi kwani ushindi upo tu bila shaka, hivyo nadhani tuache vidomo-domo na tusubiri dakika 90, tutajua nani teja wa timu hizi mbili,” alisema.

Stori na Kazija Thabit

Leave A Reply