The House of Favourite Newspapers

Mwachuo wa Ardhi Dar, Aibuka Kidedea na Mil 5 ya Magift ya Kugift, Wengine 6 Nao Waula

Balozi wa Yas Tanzania, Haji Manara (kushoto) akimpongeza Mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi Dar, Sia Mlay baada ya kuibuka mshindi wa Milioni 5 kwenye kampeni ya Magift ya Kugift. Kulia ni Afisa Mkuu Mixx by Yas, Bi. Angelika Pesha.

Dar es Salaam 29 Novemba 2024: Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya YAS, ikishirikiana  na kitengo cha Mixx by Yas, leo imekabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi 7 wa kampeni ya ‘Magift ya kugift’ kwa wiki ya 3 ambapo kati yao 6, wamejishindia  kiasi cha Shilingi Milioni 1 kila mmoja. 

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi hao Afisa Mkuu Mixx by Yas, Bi. Angelika Pesha amesema anayofuraha kuona wanakabidhi zawadi kwa washindi kwa wiki ya tatu 3 na kudai kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka.

Pesha amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milion 35 kwa washindi wa makundi  tofauti ikiwemo, mawakala, na wateja wengine.

Kwa upande wake Sia Martin Mlay ambaye amejinyakulia kiasi cha Shilingi mil. 5 ameishukuru Yas kwa  kuanzisha kampeni hiyo ya ‘Magift ya Kugift 2024’ na hatimaye yeye kuibuka mshindi, na amewaomba Watanzania kushiriki kampeni zinazoletwa na Yas Tanzania kwani hakuna ubabaishaji kila mtu anashinda kutokana na bahati yake amesema Mlay.

Nao baadhi  ya washindi wengine ambao wamejishindia zawadi ya TSh Milion 1  wameshukuru kwa kupata zawadi zao,  ambapo baadhi yao wamesema, pesa hizo wanakwenda kuziendeleza huku wengine wakiahidi kwenda kulipia ada za shule na matumizi mengine muhimu.Kampuni ya Yas imekuwa na muendelezo mzuri wa kuendesha kampeni mbalimbali ikiwa sehemu ya kujitangaza itakumbukwa kuwa kampuni ya Yas ilizinduliwa hivi karibuni awali ilikuwa ikiitwa Tigo ambayo ilidumu kwa kipindi cha miaka 30 ikitoa huduma zake hapa nchini, na kutunukiwa tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Balozi wa Yas Tanzania, Haji Sunday Manara amewataka wateja wa Yas kuendelea kufanya miamala kupitia simu zao ili waweze kuingia kwenye nafasi nzuri za kuweza kujishindia zawadi mbalimbali, na amesema Yas haina  longolongo kwenye kampeni hii, hivyo kila mtu anaweza kuibuka mshindi.