Kartra

Yassin Mustapha Arejeshwa Kumzuia Morisson

KATIKA kuhakikisha wanaizuia safu ya ushambuliaji ya Simba, iliyo na wachezaji hatari kama Bernard Morrison, kocha wa viungo wa timu hiyo raia wa Tunisia Jawab Sabri ameonekana akimpa program ya mazoezi beki wa pembeni wa timu hiyo, Yassin Mustapha.

 

Hiyo ni katika kueleka pambano hilo la watani wa jadi litakalopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.Chanzo cha habari kutoka ndani ya kambi ya Yanga, kimeliambia Championi Ijumaa kuwa kocha huyo amempa program maalum ya mazoezi binafsi katika kutengeneza fitinesi.

 

“Kama unavyofahamu Yassin hakuwepo katika timu muda mrefu akiuguza majeraha ya misuli aliyoyapata yaliyosababisha akae nje ya uwanja muda mrefu.

Tangu Jumatatu yupo kambini katika kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Simba na amerejea akiwa chini ya kocha ya viungo kwa ajili ya kutengeneza fitinesi.

 

Tunakwenda katika mchezo tukiwa tunahitaji ushindi, hivyo ni lazima wawepo wachezaji wa kazi watakaoipa ushindi timu katika mchezo huu muhimu wa kihistoria,” kilisema chanzo hicho.

 

Alipotafutwa Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidhi Saleh kuzungumzia hilo, alisema: “Yassin yupo kikosini akiendelea na mazoezi, hilo suala la kucheza au kutocheza lipo chini ya kocha Nabi.”

Stori na Wilbert Molandi,Dar es Salaam

MKUDE AJIONDOA SIMBA, HIYO SIMBA vs YANGA, KESHO HALI NI NGUMU | SOKA CHAP CHAP…


Toa comment