The House of Favourite Newspapers

Yatima Ashinda Sh. 500,000 za Gazeti la Amani

kufurahia-2

Sikitu Kyalo (kushoto) akifurahia kabla ya kukabidhiwa kitita cha shilingi 500,000/=. Kulia ni mwakilishi wa wakala wa Global Publishers wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Omary Ahmed.

 

kukabidhi-1

Mwakilishi wa wakala wa Global Publishers wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Omary Ahmed akihesabu fedha kabla ya kumkabidhi Sikitu.

kukabidhi

Omary Ahmed akimkabidhi kitita Sikitu.

kufurahia

nimepokea

Sikitu Kyalo akifurahia baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi 500,000/=.

sikitu-na-omary

Sikitu akihojiwa baada ya kujishindia kitita cha Tshs 500,000/=. Kulia ni Omary Ahmed.

SUMBAWANGA: Sikitu Kyalo (29) mkazi wa Majumba Sita katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ameibuka kidedea baada ya kushinda kitita cha shilingi 500,000 taslimu kutokana na kujibu maswali ya Chemsha Bongo katika Gazeti la Amani linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers.

Sikitu amekabidhiwa zawadi ya ushindi mjini Sumbawanga katika Mtaa wa Kiwelu majira ya saa 10:39 alasiri Jumamosi ya Oktoba 15, mwaka huu yanapouzwa Magazeti Pendwa ya Uwazi, Amani, Risasi na kushuhudiwa na mwandishi wa habari hizi.

Omary Ahmed ni mwakilishi wa wakala wa Global Publishers wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na ndiye aliyempigia simu mshindi huyo na Mohamed Larika ndiye aliyekabidhi kitita hicho.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi hiyo, Sikitu alisema alipopigiwa simu na kuelezwa amebahatika na anatakiwa kukabidhiwa fedha hizo, hakuamini kwanza, akawa anafikiri ni matapeli wanataka kumuibia tu hadi alipoambiwa aende Mtaa wa Kiwelu yanapouzwa magazeti hayo, alipokwenda akaamini kuwa ni kweli.

Baada ya kukabidhiwa fedha zake alikuwa na haya ya kusema: “Yaani hapa siamini kama Mungu ametenda maajabu kwangu leo, nimepata laki tano za bati kama naota ndoto vile…. Nawashukuru sana viongozi wa Gazeti la Amani.”
Alipotoa kauli hiyo akawa anarusha fedha hizo juu kwa furaha huku akiwashauri watu wengine kusoma gazeti hilo na kushiriki chemsha bongo inayoendelea.
Akizungumzia shughuli anazozifanya kila siku, Sikitu alisema yeye ni yatima na wamezaliwa wawili tu ambapo mdogo wake anaishi jijini Mbeya, yeye anafanya biashara ya kutembeza nguo za mitumba mkononi.

Anasema pesa aliyoipata atanunulia matofali na bati kwa ajili ya kuezekea nyumba anayotarajia kuanza kujenga wiki hii baada ya kununua kiwanja mwezi uliopita.

Na Willy Sumia, Sumbawanga

Comments are closed.