The House of Favourite Newspapers

YEMI ALADE; NIPO LEVO ZA WIZKID, DAVIDO

 

MKALI aliyewahi kutikisa na Ngoma ya Johnny 2013, Yemi Alade amesema kwa sasa muziki wake ni wa kulinganishwa na mastaa wenzake nchini humo kama vile Wizkid pamoja na Davido na kama mtu anabisha akawaulize mapromota.

 

Akizungumza na  Redio 98.3 FM, Yemi anayependa kujiita Mama Afrika alisema kuwa, amekuwa akizoea mazingira na hadi sasa ameshafanya ziara kubwa nje ya nchi kwa miaka mitatu mfululizo.

 

“Nampenda na kumthamini kila mmoja anayependa muziki. Nipo katika tano bora Nigeria, kama Wizkid na Davido wameweza kuiteka Afrika  na mimi nimeweza vivyo hivyo,” alisema Yemi Alade aliyewahi pia kutua Bongo katika Tamasha la Matumaini lililoandaliwa na Global Publishers. Mwishoni mwa mwezi huu, Yemi Alade anatarajiwa kufanya tamasha kubwa nchini Canada.

Comments are closed.