The House of Favourite Newspapers

Yondani Aibuka, Afungukia Ishu Ya Kugoma Yanga

Kelvin Yondani.

BEKI mkongwe wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, ameweka wazi kwamba atajiunga na klabu hiyo mara tu atakapokamilishiwa stahiki zake.

 

Hiyo, ikiwa ni siku chache zimepita tangu mabeki Andrew Vincent ‘Dante’ na Juma Abdul kusimamishwa na viongozi baada ya kugomea kambi ya pamoja ya timu hiyo pamoja na Yondani aliyekuwa kwenye majukumu ya Taifa Stars.

Yanga wamefikisha wiki mbili na nusu tangu walipokwenda Morogoro kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya huku nyota hao wakidaiwa kugoma kwa kudai stahiki zao.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, Yondani ameapa kutojiunga na timu hiyo hadi pale atakapolipwa stahiki zake zikiwemo za mishahara na fedha ya usajili anazodai tangu msimu uliopita.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, Yondani amefikia hatua hiyo ya kugomea kambi baada ya kuonekana kuthaminiwa wachezaji wapya na kuwasahau wa zamani wanaodai fedha zao za usajili za msimu uliopita pamoja na mishahara.

 

“Uongozi umekosea sana kwa hiki ambacho wamekifanya kwa wachezaji wa zamani ambao walitakiwa kwanza kumaliziwa malipo ya fedha zao za usajili, mishahara na posho kabla ya kuanza kutumia fedha kwa ajili ya
usajili wa wachezaji wapya.

 

“Hiyo ndiyo sababu ya msingi ya Yondani na wenzake akina Dante, Abdul ambao wamegomea kambi hiyo hadi watakapolipwa stahiki zao,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Yondani kuzungumzia hilo alisema: “Nisingependa kulizungumzia hilo kwa hivi sasa nipo Yondani aibuka, afungukia ishu… kwenye majukumu ya timu ya taifa, ni vema nikaachwa hadi hapo baadaye.

 

“Hilo la kudai stahiki lipo wazi na viongozi wanalijua ni vema wakalifanyia kazi, lakini yote kwa yote nawashauri viongozi kwa kuwaambia ni vema wakatambua mchango wetu tulioutoa sisi wachezaji wa zamani kwenye msimu uliopita, mimi nitajiunga na timu mara nitakapokamilishiwa stahiki zangu

Comments are closed.