Yondani, Ajibu Waweka Rekodi Yanga

 

BEKI na nahodha wa zamani wa Yanga, Kelvin Yondani ameweka rekodi ya kufanyiwa mabadiliko kwa mara ya kwanza msimu huu katika mchezo dhidi ya Singida United huku Ibrahim Ajibu akishinda mechi moja tu kati ya nne ambazo wamecheza kwenye ligi kuu akiwa Kapteni.

 

Yondani ni mmoja kati ya wachezaji wa Yanga ambao imekuwa ngumu kufanyiwa ‘sub’ na tangu akabidhiwe kitambaa cha unahodha mwanzoni mwa msimu huu hakuwahi kufanyiwa mabadiliko.

 

Katika mchezo na Singida uliopigwa Jumatano iliyopita alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Andrew Vicent ‘Dante’.

 

Beki huyo alipokea kitambaa kutoka kwa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyestaafu soka na Yondani awali alikuwa nahodha msaidizi lakini mapema Januari mwaka huu alivuliwa kitambaa hicho na kocha Mwinyi Zahera baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu.

Ajibu alichukua mikoba rasmi ya Yondani Januari ambapo tangu awe nahodha hadi sasa amecheza mechi nne.

Amecheza dhidi ya Mwadui FC, Taifa na kushinda mabao 3-1, akaja na Stand United akafungwa (1-0) akatoa sare na Coastal Union (1-1) na Singida United (0-0) na leo Jumapili atacheza mbele ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

 

Katika mechi hizo nahodha Ajibu amefunga bao moja pekee dhidi ya Mwadui FC kwa maana hiyo Ajibu tangu awe nahodha timu imevuna pointi tano kwenye mechi nne.

Toa comment