The House of Favourite Newspapers

Yondani Amfuata Nyosso Geita

0

GUMZO kubwa mjini Geita kwa sasa ni juu ya usajili wa nyota wa zamani wa Yanga na Polisi Tanzania, Kelvin Yondani, ambaye amesaini dili la mwaka mmoja Geita Gold, mkataba utakaomfanya kuziba safu ya ulinzi sambamba na Juma Nyosso ambaye tayari ameingia kwenye klabu hiyo.


Yondani aliachana naYanga
mwanzoni mwa msimu wa 2019/20 na baadaye akajiunga na Polisi Tanzania baada ya kupita miezi sita mkataba uliodumu kwa mwaka mmoja kabla ya kuamua kujiunga na Geita Gold.


Akizungumza na
Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo, amesema, ni kweliYondani
ataungana na Juma
Nyosso msimu huu baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja, kwani wao wameamua
kutengeneza ukuta
wa kudumu ili waweze kufikia malengo yao.


“Tarifa ya faraja kwetu ni uwepo wa
wachezaji hawa wazoefu, kwani ni kweli Yondani atakipiga msimu huu sambamba na Nyosso ikiwa ni sehemu ya maboresho ya safu yetu ya ulinzi.


“Mbali na hivyo pia tayari tumefanikiwa
kumsaini Ditram Nchimbi, hivyo utaona hitaji la timu yetu lilikuwa ni kupata zaidi wachezaji wenye uzoefu na ligi ili tuweze kufikia male, pamoja na wote kusaini mwaka mmoja mmoja, ni wazi kwamba kama watatuwezesha kufikia malengo yetu ni wazi wataongeza tena,” alisema Kivuyo.


Wakati huohuo, uongozi wa timu ya Geita
Gold FC umethibitisha kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wenye thamani ya Sh milioni 500

STORI: MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

Leave A Reply