The House of Favourite Newspapers

Yondani Azua Taharuki Moro, Viongozi Watuliza Mzuka

Kelvin Yondani.

JANA Alhamisi nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani alizua taharuki baada ya kushindwa kutokea mazoezini lakini uongozi wa timu yake ukaweka mambo sawa kuwa nyota huyo ana matatizo ambayo yalimlazimu abakie hotelini.

 

Yondani alikosa mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia mkoani hapa, hivyo kuzua taharuki wakati wa kuelekea mechi ya timu hiyo dhidi ya Simba, wikiendi hii. Taarifa za uhakika ambazo Championi Ijumaa lilizipata baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo ni kuwa Yondani alibaki hotelini kwa ajili ya kumaliza matatizo ya familia yake ambayo alikuwa nayo.

 

“Yondani ni mzima kabisa wala usihofu lolote juu yake kutokana na kutoonekana kwenye mazoezi ya leo (jana), ila fahamu kwamba hana shida yoyote ile na atakuwepo kwenye mchezo ujao dhidi ya Simba. “Kilichotokea kwake ni kwamba alipata tu matatizo ya kifamilia hivyo akahitaji muda wa kuyatatua ndiyo maana akabakia hotelini, lakini kesho (leo) ataungana na wenzake kwa ajili ya kuendelea na mazoezi,” alisema mmoja wa viongozi wa timu hiyo.

Comments are closed.