Yondani, Dante Waibua Mapya Yanga

Kelvin Yondani

MASHABIKI ambao hawakauki kwenye mazoezi ya Yanga mjini hapa, wamedai hata mabeki wao wa kati, Kelvin Yondani, Andrew Vicent ‘Dante’ na Juma Abdul wasipokuwepo Yanga itanoga msimu ujao.

 

Wachezaji hao watatu hadi jana walikuwa hawajaripoti kambini kwa sababu mbalimbali. Kwenye nafasi ya mabeki wa kati ambayo hucheza Yondani na Dante hadi sasa ina zaidi ya wachezaji wanne huku upande wa Abdul pia kukiwa na wachezaji watatu.

Beki wanaoweza kucheza kati kwa maana kwenye nafasi ya Dante na Yondani ni Mustapha Suleiman raia wa Burundi, Lamine Moro raia wa Ghana, Ally Mtoni ‘Ally Sonso’ na kijana Cleophace Sospeter.

 

Wakati upande wa kulia anapocheza Juma Abdul kuna Ally Ally na Paulo Godfrey ‘Boxer’. Kwa mujibu wa mashabiki hao ambao wamekuwa hawakauki kwenye Viwanja vya Bigwa asubuhi na jioni, wamedai hadi muda huu hawaoni pengo la Yondani, Dante na Abdul.

 

“Kwa sasa hatuna homa kama msimu uliopita wakikosekana, kusema kweli hapa tuendelee kumpongeza Zahera kwa kuliona hili kwani bila hivyo tungekuja kufa na presha hasa sasa ukiangalia tangu timu iingie kambini wachezaji hawa hawapo,” walisikika mashabiki waliokuwa wamekaa kundi kubwa.

 

Katika mechi na Moro Moro Kids iliyochezwa Uwanja wa Highlands Park nje kidogo ya Morogoro mjini walionyeshwa kuridhishwa na mwanzo wa muunganiko wa wachezaji hao.

Nafananishwa na JUX/ ALIKIBA na DIAMOND /siwezi


Loading...

Toa comment