The House of Favourite Newspapers

Yondani: Huyu Kindoki Ni Hatari Sana

Kelvin Yondani

BEKI mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani amesifu kiwango kilichoonyeshwa na kipa wa timu hiyo, Mkongoman, Klausi Kindoki huku akimtaka kutobweteka.

 

Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache tangu kipa huyo aonyeshe kiwango kikubwa cha kuokoa michomo ya Namungo FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Heritier Makam­bo.

 

Awali, kipa huyo alikuwa akikaa benchi katika michezo ya ligi na michuano waliy­okuwa wanashiriki kutokana na kubez­wa kiwango chake lakini juzi alionyesha uwezo wa kushangaza.

Akizungumza na Championi Jumatano, Yondani alisema kuwa Kindoki ni kipa mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kudaka, lakini presha ya mashabiki ndiyo imemfanya apoteze hali ya kujiamini akiwa golini.

 

“Kindoki siyo kipa mbaya ni mzuri na nilianza kumuo­na tangu alipojiunga na Yan­ga mwanzoni mwa msimu huu, kosa kubwa alilolifanya aonekane siyo mzuri ni kupoteza hali ya kujiamini baada ya kufungwa mich­ezo ya mwanzoni, lakini sasa amesha­waonyesha watu kuwa yeye ni hatari sana.

 

“Anachotakiwa ni kuwajua mashabiki na kuongeza hali ya ku­jiamini ili akontroo presha kama alivyofanya katika mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho tulipocheza na Namungo, kikukweli alidaka vizuri,” alisema Yondani.

Stori na Wilbert Molandi

Comments are closed.