The House of Favourite Newspapers

YONDANI: MKINILETEA HUYU WAMEKWISHA

BEKI mkongwe wa kati na nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani amesema akisajiliwa mlinzi wa Rayon Sports ya Rwanda, Abdoul Rwatubyaye safu yao itatisha sana na watakata ngebe za washambuliaji jeuri kama, Emmanuel Okwi.

 

Lakini sasa unajua kilichotokea, Yanga wametua kwa meneja wa mchezaji huyo na dau ambalo limemshtua ikabidi awaangalie usoni halafu acheke kwanza. Halafu akawauliza; “Hivi kweli kwa akili yenu, mchezaji mkali

 

 kama huyu mnaeza kumpata kwa dola elfu 40? Acheni masihara ongezeni mzigo.” Yanga imepeleka ofa hiyo ya dola 40,000 (Sh.milioni 91) lakini wameambiwa angalau waongeze ifike dola 60,000 (Sh137milioni) bado wanajifikiria. Spoti Xtra limejiridhisha kwamba kwenye mkataba wa mchezaji huyo kuna kipengele kinachosema kama akipata timu lazima ailipe Rayon Dola 50,000 na tayari Vita Club ya DR Congo imeanza kumnyemelea.

 

Yondani ambaye ana mke halali na watoto watatu, alisema kwamba anafahamu vizuri uwezo wa beki huyo mwenye umbo kubwa ambaye alimuona wakati timu hiyo ilipocheza na Rayon katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho.

 

Yondani alisema, siyo mchezaji mbaya ni mzuri mwenye uwezo anayeendana naye katika aina ya uchezaji katika nafasi ya ulinzi inayochezwa hivi sasa na yeye, Andrew Vicent na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

“Niwe muwazi yule beki ni mzuri mwenye sifa zote za kucheza beki wa kati, kwani ana umbo kubwa la kucheza mipira ya juu kwa kupiga vichwa, hivyo ni beki anayehitajika Yanga.

 

“Kwa jinsi nilivyomuona katika mechi tuliyokutana nao ya kimataifa, alijitahidi kuwadhibiti washambuliaji wetu Makambo (Heritier) na Mahadhi (Juma) akitumia vizuri umbo lake.

“Ninaamini kama akitua Yanga, basi wale washambuliaji jeuri watakiona kwani tutakuwa tuna safu nzuri ya ulinzi itakayoleta ushindani,” alisema Yondani ambaye makazi yake ni Kigamboni.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

WANACHAMA Simba Wapewa MashartI/ Uchaguzi Wapamba Moto

Comments are closed.