Yondani, Sonso Kuibukia Moro

NYOTA wa timu ya Yanga ambao walikuwa na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyokuwa ikishiriki michuano ya Afcon, kesho Alhamisi wanatarajia kuingia kambini baada ya kumaliza mapumziko ya siku 14.

 

Nyota hao ni Kelvin Yondani, Ally Mtoni ‘Sonso’, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambao walipewa mapumziko ya siku 14 baada ya kurudi hapa nchini kutokana na Taifa Stars kutolewa hatua ya makundi bila ya kuambulia hata pointi moja.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten, alisema kuwa wachezaji ambao hawakuwa na majukumu ya timu ya taifa, wote wamewasili kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao. “Tayari wachezaji wote wamewasili kambini mkoani Morogoro, ambapo maandalizi yetu yanafanyika.”

VIKOSI Vitatu vya Simba Hivi Hapa kwa Mifumo Yote


Loading...

Toa comment