The House of Favourite Newspapers

Young Killer na Mkenya Kukinukisha Leo Dar

RAPA anayefanya vizuri Bongo, Young Killer na msanii Khaligraph Jones kutoka nchini Kenya wanatarajia kukinukisha kwa kusherekea Kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ‘Happy Birthday’ ya Young Killer sambamba na uzinduzi wa Wimbo wa Shots ambao wameshirikiana.

 

Killer amesema uzinduzi wa Video ya Shots utafanyika katika Ukumbi wa Club Next Door, Masaki Jijini Dar, leo usiku na kuwaomba mashabiki kumpokea kwa ujio mpya akiwa chini ya Kampuni ya Wanene Entertainment.

“Nimekuja upya kwa kusherehekea Birthday yangu na kuzindua Video ya Shots niliyoshirikiana na Khaligraph kutoka Kenya. Nawashukuru Wanene kwa kunipa nafasi katika kampuni yao, leo nimejipanga kufanya makubwa kwenye uzinduzi,” alisema Young Killer.

 

Kwa upande wa Khaligraph amesema alikuwa anatamani kufanya ngoma na Killer. “Namkubali sana Young Killer, nilikuwa natamani kufanya naye kazi, miaka kama miwili iliyopita tulizungumza na hatimaye leo nimefika Tanzania kwa ajili ya uzinduzi wa kichupa chetu. naahidi kufanya bonge la shoo, OG,” alisema Khaligraph.<iframe width=”640″ height=”360″ src=”https://www.youtube.com/embed/mUAVp5uzN-s” frameborder=”0″ allow=”autoplay; encrypted-media” allowfullscreen></iframe>

Comments are closed.