The House of Favourite Newspapers

Young Thug ana Kolabo ya Nyimbo 40 na Kanye West

0

young-thug-kanye-westYoung Thug na Kanye West.

RAPA Young Thug amefunguka kuwa mpaka sasa ana nyimbo 40 ambazo amerekodi na rapa mwenzake ambaye swahiba wake, Kanye West.

Thugger alianika ubuyu huo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na “The Angie Martinez Show” wikiendi iliyopita ambapo alfunguka kuwa yeye na West ambaye ni kiongozi wa kampuni ya G.O.O.D. Music, wamefanya nyimbo zipatazo 40 amabazo ni zaidi ya albamu.

“Mimi na yeye, tumefanya nyibo nyingi sana, mashairi kibao pia tumefanya,” alisema Thugger. Aliongeza pia kuwa yeye na Kanye wamekuwa wakifanya kazi pamoja kwa miaka mitatu sasa.

 

Hadi sasa haijafahamika vizuri kama kuna wibo wowote kati ya hizo utakuwemo kwenye albamu mpya ya Kanye “Waves” au amezitunza kwa ajili ya projekti nyingine ya tofauti. “Ninadhani tutaziweka zote pamoja, siwezi kuwaambia ni siku gani tutafanya hivyo kulingana na mkataba niliosaini naye.” Alisema Thugger.

 

Young Thug anatarajia kuachia mixtape yake ya Slime Season sehemu ya tatu Februari 5.

Leave A Reply