The House of Favourite Newspapers

Youssou n’dour anaogelea kwenye utajiri

0

Mwanamuziki kutoka nchini Senegal, Youssou N’Dour. 

YOUSSOU N’dour ni mwanamuziki kutoka nchini Senegal barani Afrika. Anatumia staili Mbalax ambao ni mchanganyiko wa lugha za asili nchini Senegal ikijumuisha rhumba, jazz, rocky, pop na soul.

Jarida la People With Money la Afrika Magharibi limemtaja kwa mara nyingine kuongoza kwa utajiri mwaka 2015 kwa upande wa wasanii wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola milioni 145 (zaidi ya shilingi bilioni 319).

Kupitia muziki wake anamiliki majengo makubwa, vyombo vya habari (redio na runinga), migahawa na utengenezaji wa vyakula, lebo ya muziki na mavazi, timu ya mpira wa miguu, vinywaji vikali na siasa ambapo mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Utamaduni.

Leave A Reply