The House of Favourite Newspapers

A-Z BABA KICHUYA ALIVYOTEKWA – VIDEO

 

MOROGORO: Baba wa Mcheza Soka wa Timu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club na Taifa Stars, Shiza Kichuya, Ramadhani Kichuya ambaye ni dereva wa teksi maeneo ya Msamvu mjini Morogoro hivi karibuni yamemfika mazito baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.

 

NI JUMAPILI ILIYOPITA

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita saa nne usiku huku yakiwepo madai kwamba, aliwekewe sumu kwenye kinywaji kabla ya kutekwa.

 

TAARIFA ZA AWALI

Awali, juzi Jumatatu asubuhi zilipatikana taarifa kwamba, kuna mtu ameonekana akiwa hajitambui katika mashamba ya SUA, maeneo ya Mafinga ambapo mwandishi wetu aliwasha pikipiki yake hadi eneo hilo lakini alipofika akakuta tayari mtu huyo ameshachukuliwa na gari la polisi.

 

NI BABA KICHUYA

Mwandishi wetu akiwa eneo hilo alisikia watu wakijadili tukio hilo la kinyama huku aliyefanyiwa akitajwa kuwa ni baba wa mwanasoka Shiza Kichuya.

“Dah! Ni baba yake Kichuya bwana, inaonekana ametekwa huko, wakamfanyia walichofanya kisha wakaja kumtupa hapa akiwa hajitambui, ni kama mtu aliyeleweshwa hivi, yaani watu bwana hawana huruma kabisa,” alisema kijana mmoja aliyeonekana kuguswa na tukio hilo.

 

APELEKWA HOSPITALI

Ikaelezwa kuwa, baada ya polisi kufika walimchukua na kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu kabla taratibu nyingine za kisheria hazijafuatwa.

MWANDISHI ATINGA HOSPITALI

Kufuatia maelezo hayo, mwandishi wetu alifunga safari hadi hospitalini hapo na kufanikiwa kumkuta baba Kichuya akipatiwa matibabu huku akiwa na hali mbaya.

 

MWANDISHI AWAACHA MADAKTARI

Kufuatia mazingira hayo, mwandishi wetu kwa kutumia busara aliamua kuondoka ili kuwapa nafasi madaktari waendelee kumhudumia ambapo alifika tena kesho yake (Jumanne) na kufanikiwa kuongea naye.

 

HUYU HAPA BABA KICHUYA

“Kama unavyojua mimi ni dereva wa teksi pale Msamvu, sasa jana (Jumapili) majira ya saa 4 usiku nilikodiwa na abiria watatu wakaniambia niwapeleke Baa ya Rombo White, nikiwa njiani wakanitaka tuingie kwanza Baa ya Royas wapashe.

“Kwa kuwa walikuwa wamenikodi, nikaona sawa, tukaingia kwenye baa hiyo, wakaagiza bia na mimi kwa kuwa sinywi pombe wakaniagizia soda, tukakaa sana pale. Nilipoenda chooni kujisaidia huku nyuma nadhani waliniwekea madawa ya kulevya, nikalewa nashtuka niko wodini, sijui gari yangu na simu yangu viko wapi.”

 

PATRONI AFUNGUKA

Patroni wa hospitali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Edwin Damas alithibitisha kumpokea Kichuya akiwa hajitambui na kusema wamepambana kuhakikisha wanamrudisha kwenye hali nzuri.

“Ni kweli jana asubuhi tulimpokea akiwa hajitambui baada ya kulishwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni sumu na tulifanya jitihada za kuikata sumu hiyo, tumefanikiwa kama unavyomshuhudia amezinduka na anaendelea vizuri,” alisema mhudumu huyo.

 

KICHUYA ATAFUTWA

Kufuatia tukio hilo, mwandishi wetu alimpigia simu Shiza Kichuya ambapo alipoulizwa kama ana taarifa za kilichompata baba yake alisema anazo lakini kwa wakati huo alikuwa Dar akiwasiliana na watu wa Moro kuhakikisha gari la baba yake linapatikana.

“Shekidele mimi nimerudi jana (Jumatatu) kutoka Lethoto, taarifa za kilichompata baba ninazo, nimezipata jana mchana, niko njiani nakuja huko Moro lakini kwa sasa naendelea kufanya juhudi gari la baba lipatikane, nikifika Moro nitakupigia,” alisema winga huyo machachari wa kushoto wa Timu ya Simba na Taifa Stars.

Jumapili iliyopita saa nne usiku huku yakiwepo madai kwamba aliwekewa sumu kwenye kinywaji kabla ya kutekwa.

Comments are closed.