The House of Favourite Newspapers

A-Z FIESTA ILIVYOFUNIKA DAR (PICHA +VIDEO)

Msanii Maua Sama (kulia) na wacheza shoo wake wakitoa burudani.

MSIMU wa Fiesta 2018 uliokuwa na Kaulimbiu ya Vibe kama Loteee, licha ya awali kutaka kuingia dosari kwa kutofanyika jijini Dar mwaka huu, hatimaye tamasha hilo limefanyika na kufunika mwanzo-mwisho, Ijumaa Wikienda lilikuwepo linakupa A-Z lilivyokuwa.

Mwanamuziki  wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’,  akifanya yake usiku wa kuamkia jana katika Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lootee usiku wa kuamkia leo katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar.

VIWANJA VYA POSTA VYAFURIKA

Tukio hilo la kihistoria lilihitimishwa rasmi kwenye Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama jijini Dar, palipofurika, usiku wa kuamkia jana ambapo lilinoga ile mbaya tofauti na wengi walivyofi kiri.

Katika tamasha hilo, pamoja na kupambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipanda jukwaani na kuwapa ofa mashabiki waliofurika kwenye tamasha hilo si tu kwa kujirusha hadi asubuhi, bali aliwapa ruhusa ya kujirusha kwenye tamasha hilo kwa siku tatu mfululizo usiku na mchana kama wataweza.

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wanaounda kundi la Rostam —  Roma (katikati) na Stamina pamoja Maua Sama — wakifanya yao.

MAKONDA AMTAJA RUGE KAMA SHUJAA Sambamba na hilo, Makonda alipopanda jukwaani alielezea simanzi yake kwa kufanyika tamasha hilo bila uwepo wa mmoja wa waanzilishi wake, Ruge Mutahaba aliyeko nchini Afrika Kusini kwa matibabu huku hali yake ikiwa na usiri mkubwa.

Makonda alimuelezea Ruge ambaye ni Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti wa Clouds Media, kama shujaa katika tasnia ya burudani ya muziki nchini na kuwashauri waliosaidiwa naye wasisite kumpa shukrani. Aliwataka waliosaidiwa na Ruge kuachana na wachache wanaopenda kumlaumu mtu huyo kwa jambo ambalo pengine halistaili lawama.

Umati wa mashabiki ukiwashangilia Alikiba na kundi lake.

MAOMBI YA RUGE Baada ya kusema hayo, Makonda aliongoza maombi ya kumuombea Ruge na kumtakia afya njema ambapo baadhi ya mashabiki walionekana kutokwa na machozi. Baada ya maombi hayo, burudani ilien

delea ambapo kabla ya Makonda, Chid Benz, Mariyoo na Neddy Music walikuwa wameshafungua pazia la burudani. Uhondo huo uliokuwa umekatishwa na Makonda uliendelea tena ambapo Rich Mavoko alivamia jukwaa na wanenguaji wake kisha kuanza kuliamsha.

PIGA NIKUPIGE Hapo ilikuwa ni kama piga nikupige maana Chegge kutoka TMK Wanaume Family, Rosa Ree, Vee Money nao walikiwasha ile mbaya. Wasanii hao baada ya kuwachezesha mashabiki, Fid Q naye alipanda jukwaani ambapo kabla hajashuka Mkali wa Masauti, Christian Bella ‘Obama’ alimfuata na kuanza kukamua naye wimbo wa pamoja huku wakipigiwa vyombo laivu, hali iliyoongeza ladha kwenye tamasha hilo.

Mashabiki wakiwa wameshikika.

SHANGWE LA KIBA Baada ya Bella, Alikiba na Abdu Kiba walipanda na kundi lao la Kings Music ambapo bila kupepesa walifunika ile mbaya na kusababisha shangwe kubwa. Mamaa Chura, Snura Mushi, kama kawaida yake naye alivamia jukwaa akiwa na wanenguaji wake matata waliokuwa wakiwanogesha mashabiki kwa staili mbalimbali ikiwemo ile ya chura na  kuchuma mchicha. Wanenguaji hao walionekana kuwatoa udenda wanaume wakware waliokuwa macho kodo kuangalia nyonga jukwaani.

WEUSI KAMA KAWAIDA YAO Baada ya burudani ya kuangalia nyonga,

wagumu wa Kundi la Weusi likiwa na wasanii wake, Nikki wa Pili, G Nako, Joh Makini na Lord Eyez nao walivamia jukwaa na kudhihirisha kilichowatoa Arusha kuzama Dar maana makamuzi yao yalikuwa kama kawaida yao. Wanamuziki wanaokuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Fleva, Whozu na Zaiid, nao walionesha kasi yao wanayokuja nayo ambapo ilikuwa kama wanawawashia taa nyekundi wanamuziki walioko kwenye chati kwa sasa.

MNYAMA NA STAILI ZAKE

Wengine waliofunga kazi kwenye onesho hilo ni Khalid Mohammed ‘T.I.D Mnyama wa Unyamani’ ambaye alivamia jukwaa na kuonesha umahiri wake wa kulitawala jukwaa kwa staili zake za kujinyonganyonga. Maua Sama anayetamba na Kibao cha Iokote ambaye alipanda jukwaani kukiwa kumeshapambazuka, ilikuwa ni kama alikwenda kuwapa dozi mashabiki waliochoka na mkesha maana uwanja mzima ulianza kulipuka kwa mayowe huku mashabiki hao wakiimba kibao hicho sambamba naye.

 

CHID BENZ NA BLUE

Tamasha hilo lilihitimishwa asubuhi ya jana na shoo ya pamoja kati ya Chid Benz aliyerudi jukwaani mara ya pili na Mr Blue ambao walihitimisha kibabe na kusababisha kundi la mashabiki kuwasindikiza mpaka nje ya viwanja hivyo huku wakiwamwagia sifa kwa shoo yao. Hivyo ndivyo Fiesta ya mwaka huu ilivyohitimishwa na kuacha bonge la shangwe kwa mashabiki wa burudani.

STORI NA RICHARD BUKOS – GPL

Comments are closed.