A-Z MZEE YUSUF ALIVYOVAMIWA NA MAJAMBAZI

Alhaj Mzee Yusuf na Mkewe Leila Rashid

DAR ES SALAAM: Mwaka umeanza vibaya kwake! Unaweza kusema maneno hayo baada ya aliyekuwa mwimbaji na kiongozi wa zamani wa Kundi la Jahazi Modern Taarab aliyemrudia Muumba wake, Alhaj Mzee Yusuf kuvamiwa na majambazi, Amani linakupa A-Z ya tukio hilo.  

 

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu nyumbani kwake Chanika Buyuni Wilaya ya Ilala jijini Dar ambapo majambazi hao walivamia na kufanya umafia ikiwemo kumjeruhi mkewe Leila Rashid sehemu mbalimbali za mwili wake. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari majambazi hao walipofika kwenye nyumba hiyo waliruka ukuta  kabla hawajaingia pale nje walikutana na Alhaj Mzee ambapo jambazi mmoja mwenye silaha alimdhibiti.

 

Kutokana na kudhibitiwa huko Mzee Yusuf naye aliamua kupambana na jambazi huyo huku akipiga kelele kuomba msaada kwa majirani. Majambazi wengine wawili waliingia ndani na kuanza kupiga watu wakati wakitafuta walivyofuata ambapo katika tukio hilo walimjeruhi mke wa Mzee Yusuf baada ya kumshambulia kwa nondo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumuumiza hasa kichwani na mapajani.

 

Akizungumza na Amani, Mzee Yusuf alikiri kuvamiwa na mkewe ndiye aliyejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili. “Ni kweli nimekumbwa na majanga ya kuvamiwa na majambazi na hivi tunavyoongea (Jumatatu iliyopita) niko hospitali hapa Chanika nahangaika na hali ya mke wangu ambaye ameumia.

 

“Unajua baada ya kuvamiwa mke wangu aliwaonesha upinzani mkali kwa kupambana nao hivyo walivyomuona mbishi walimpiga sana nondo za kichwani, mbavuni na mapajani wakati huo mimi nikipambana na jambazi mmoja kule nje ambaye naye alikuwa na bastola lakini niligundua ni zile zinazotumika kupigia baruti.

 

“Nilijaribu sana kupiga mayowe na kuwaita majirani na kuwaambia waje kutoa msaada baada ya kuwabaini kuwa hawakuwa na silaha za maana lakini majirani zangu wote waliogopa kutoka hivyo tulipambana peke yetu,” alisema Mzee Yusuf.

Mzee Yusuf alisema majambazi walichukua vitu vingi ambavyo idadi yake hajaijua mara moja zikiwemo pesa shilingi laki tano, simu aina ya i-phone yenye thamani ya shilingi laki tano, saa yake ya mkononi yenye thamani ya shilingi laki tano, pete tatu za madini ya Silva zenye thamani ya shilingi laki moja na nusu kila moja.

 

Pamoja na hivyo, walichukua pia vitu vingine vidogovidogo yakiwemo mabegi ya nguo za watoto, mabegi ya shule yaliyokuwa na vifaa vya shule na vingine vingi. “Muda mfupi baada ya majambazi hao kuondoka nilipiga simu polisi ambapo baada ya kama nusu saa walifika na kuanza kufanya uchunguzi wa awali kisha kuwafuatilia walipoelekea,” alisema Mzee Yusuf. Tukio hilo liliripotiwa Kituo cha Polisi cha Chanika na kufunguliwa jalada namba CNK/144/2019 UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

KARIBU ujiunge na familia ya marafiki wa Global TV Online – Club sasa, uwe wa kwanza kupata video zote za Global TV, video za hamasa kutoka kwa Eric Shigongo, breaking news za matukio yote duniani, michezo na dondoo za afya. Utapata nafasi ya kuingia bure na kutazama shoo, matamasha, semina na burudani zinazoandaliwa na Global TV mikoa yote Tanzania.
Pia, ukiwa na tatizo la kifamilia mfano misiba, kuuguliwa na majanga, marafiki zako wa Global TV Club tutakusaidia.
 
Pia, tutakuunganisha na mtandao wa marafiki zetu waliyofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, ili upate mafunzo maalum ya kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment