A-Z Safari Ya Lulu Kutoka Uraiani Kwenda Gerezani (Pichaz + Video)

Mwigizaji wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ (kulia) akiongea neno na Muna Alphonce nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo kabla ya kuingia kizimbani.
…Akielekea ndani ya mahakama.
…Akiwa ndani ya mahakama (aliyeinama).
Mama Kanumba, Flora Mtegoa (wa tatu kulia) akifuatilia kesi.
Watu waliokuwa ndani ya mahakama leo.
Wanahabari (kulia) wakichukua matukio.
Lulu akitafakari jambo baada ya kutiwa hatiani kwa kuua bila kukusudia ambapo alihukumiwa kwenda jela miaka miwili.
Ndugu zake Lulu wakilia huku wakitoka nje ya mahakama baada ya hukumu kutolewa.
Mama Kanumba (wa pili kulia) akitoka nje ya mahakama.
Mama yake Lulu, Lucreasia Kalugira (wa pili kushoto) akilia baada ya hukumu hiyo.
…Akiwa haamini kilichotokea.
Muna Alphonce akitoka mahakamani.
Mwanasheria wa Lulu, Peter Kibatala, akiwasiliana na mawakili wenzake kuhusu jambo walilopanga kufanya baada ya hukumu hiyo.
Ndugu zake Lulu wakiondoka mahakamani.
Karandinga lililombeba Lulu kumpeleka gerezani.
Mwanahabari wa mtandao huu, Denis Mtima (wa kwanza kulia, aliyeelekeza uso kwenye kamera) akitafakari jambo baada ya hukumu.
Watu mbalimbali waliofika mahakamani hapo wakiwa tayari kuondoka.

MWIGIZAJI Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo amehukumiwa kwenda jela miaka miwili na Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa mwigizaji wa filamu, Steven Kanumba.  Kifo cha Kanumba kilitokea Aprili 7, 2012 nyumbani kwake Sinza-Vatican jijini Dar es Salaam na mazishi yake kufanyika makaburi Kinondoni.

Mbali na hukumu ya leo kwa staa huyo, aliwahi muda mrefu rumande kabla ya kupewa dhamana.  Hata hivyo, wakili Peter Kibatala amesema atakata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu hiyo.

(PICHA: RICHARD BUKOS/GPL)

HUKUMU YA LULU INATOLEWA LEO!!! MTAZAME ALIVYOTINGA MAHAKAMANI!

 

BREAKING: LULU AKIPELEKWA GEREZANI NDANI YA DIFENDA!

MAMA KANUMBA BAADA YA HUKUMU AKIMBILIA MAKABURINI!

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment