Zabibu Afunguka Sababu za Kutoingia Mitandaoni

DADA wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Ali Salehe Kiba ‘King Kiba’, Zabibu Kiba, kwa mara ya kwanza amefunguka sababu inayomfanya asiwe mtu wa kuingia mara kwa mara mitandaoni kama ilivyo kwa dada wa mastaa wengine.
Akichezesha taya na Gazeti la IJUMAA, mrembo huyo asiyekuwa na skendo mitandaoni alisema kuwa, muda mwingi anautumia kufanya mambo yake mengine yanayomuingizia kipato, lakini pia amekulia katika mazingira ya kutoweka mambo yao hadharani.
“Unajua aina ya maisha niliyokulia ndiyo yanayonifanya nisiwe mpenzi wa kuingia mitandaoni, lakini pia muda ambao siingii huko nakuwa nafanya mambo yangu mengine ambayo yananiingizia kipato, hivyo niwatoe tu hofu mashabiki wangu kuwa kuanzia sasa wataniona kwa sababu nipo mbioni kufungua biashara,” alisema Zabibu.
STORI: MEMORISE RICHARD

