Zabibu Asimulia Mumewe Banda Alivyonusurika na Xenophobia Sauz

MKE wa beki wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga Highlands Park FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda, Zabibu Kiba ameibuka na kuweka wazi hali ya mumewe huyo ambaye yuko Sauz ambako kuna machafuko ya Xenophobia.

 

Machafuko yanayoendelea nchini Afrika Kusini ya kiubaguzi yalianza Jumapili iliyopita ambapo raia wa nchini humo wamekuwa wakivamia maduka ya raia wa kigeni na kuanza kupora mali na kuchoma moto ikiwa ni pamoja na kuua watu kadhaa.

 

Banda amekuwa nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu akicheza soka la kulipwa ambapo awali alikuwa akikipiga katika klabu ya Baroka kabla ya msimu huu kutua Highlands Park iliyopo Mji wa Johannesburg huku machafuko yakiwa yametokea katika Mji wa Cape Town.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Zabibu alisema kuwa, Banda hajapatwa na matatizo ya aina yoyote kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo kwani yeye yupo mji mwingine.

 

“Mimi nipo huku Tanzania lakini mume wangu yupo huko Afrika Kusini na nimewasiliana naye, wala hana shida yoyote kwa kuwa sehemu iliyotokea machafuko siyo ile anayoishi yeye, kikubwa namuombea Mungu aweze kuwa salama,” alisema Zabibu.


Loading...

Toa comment