Zaha Akimbia Timu ya Taifa Ivory Coast

STAA wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ameomba asijumuishwe  kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kinachojiandaa na michezo ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Cameroon na Msumbiji.

 

Kocha wa Ivory Coast Patrice Beaumelle amesema Zaha huwa anaumwa kila anaporudi kutoka kwenye majukumu ya taifa hilo, na anaendelea kutafakari juu hatma yake kwenye soka la Kimataifa.

 

“Ameomba tusimjumuishe kwa sababu anarudi nyumbani akiwa anaumwa kila anapotoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa” amesema kocha Beamelle.

 

Zaha ambaye alibadili uraia mwaka 2017, baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha England, ameichezea Ivory Coast mechi 21 na kufunga magoli 5.2177
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment