Zahera Aanza na Gia Mpya Yanga

Mwinyi Zahera

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amepanga kuingiza gia mpya kwenye mechi za mikoani kuanzia wiki ijayo kwani baada ya mechi na Mwadui ya Shinyanga jijini Dar es Salaam Jumanne watakwenda huko.

 

Yanga italazimika kuanza mzunguko wa pili kabla haijamaliza mzunguko wa kwanza baada ya kiporo cha Azam kuwekwa pembeni. Baada ya mechi na Mwadui, Yanga itakwenda Shinyanga kucheza mchezo wake wa kwanza mkoani katika mzunguko wa pili dhidi ya Stand United.

Yanga inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 50 ikiwa imecheza michezo 18 ya ligi ikishinda michezo 16 na kutoa sare michezo miwili . Akizungumza na Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema Zahera ameweka nguvu kubwa kwenye mechi za mikoani na kuhakikisha kila mchezo anaingia na gia mpya na lazima ushindi upatikane kote.

 

“Moja ya malengo ya mwalimu ni kuona timu inafanikiwa kushinda mechi zake zote za mikoani kwa kuanzia na Stand United ambayo tutakwenda kukutana nayo baada ya mchezo wetu dhidi ya Mwadui ,” alisema Saleh.

STORI NA KHADIJA MNGWAI

Loading...

Toa comment