The House of Favourite Newspapers

Zahera Aendeleza Ubabe Yanga

Kocha wa Yanga, Mkongo, Mwinyi Zahera.

KOCHA wa Yanga, Mkongo, Mwinyi Zahera ameendelea kuweka rekodi ndani ya kikosi hicho baada ya kumzidi aliyekuwa kocha wa timu hiyo, George Lwandamina kwa mafanikio ya mzunguko wa kwanza. Lwandamina raia wa zambia, alikuwa akiinoa Yanga msimu uliopita na aliondoka katikati ya msimu kutokana na klabu kushindwa kumtekelezea mahitaji yake.

 

Msimu uliopita Yanga ikiwa chini Mzambia huyo, baada ya kucheza mechi 5 za mzunguko wa kwanza, ilivuna alama 28 tu kwa kushinda mechi saba na kutoa sare saba na kupoteza mechi moja dhidi ya Mbao FC.

Mechi ambazo alishinda Mzambia huyo ilikuwa Yanga dhidi ya Mbeya City (5-0), Azam FC (1-2), Njombe Mji (0-1), Kagera (1-2), Ndanda (1-0), Stand United (0-4) na Ruvu Shooting (0-1).

 

Lakini msimu huu mambo yamekuwa tofauti kidogo kwa Yanga ambayo inaongozwa na Mkongo kwani imecheza mechi 18 na kusaliwa na mechi moja dhidi ya Azam kumaliza mzunguko wa kwanza na imevuna alama 50.

 

Zahera ameweka rekodi katika hizo mechi 18 ambazo timu yake imecheza, ametoa sare mbili pekee na kushinda 16 na sita kati ya hizo akicheza nje ya Dar es Salaam na anashikilia usukani wa Ligi Kuu Bara. Msimu huu Ligi Kuu Bara ina timu 20, msimu uliopita zilikuwa 16.

MARTHA MBOMA

Comments are closed.