The House of Favourite Newspapers

Zahera aleta kiberenge kama Msuva Jangwani

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera yuko kwenye hatua za mwisho kumalizana na winga kiberenge mwenye kasi aina ya Simon Msuva ambaye ni raia wa Kongo.

 

Zahera ameliambia Spoti Xtra kwamba, Yanga inataka kumsajili winga huyo kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao katika usajili wa dirisha dogo linalofunguliwa Novemba 15, mwaka huu.

 

Licha ya kutotaja kwa majina na klabu walizopo kwa sasa, Zahera aliwataja wachezaji hao anaotaka kuwaongeza ni kiungo mmoja, washambuliaji wawili na winga mmoja.

 

“Tayari nimeshakamilisha ripoti yangu ya usajili, ninataka kusajili wachezaji wanne tu kati ya hao yupo kiungo mmoja mkabaji, washambuliaji wawili na winga mmoja.

 

“Winga huyo ninayetaka kumleta ni mwenye kasi na pumzi za kutosha atakayeanzisha mashambulizi na kuzuia ndani ya wakati mmoja, pia mwenye uwezo mkubwa wa kupiga krosi na kufunga mabao ambaye hivi sasa hayupo Yanga.”

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

WANACHAMA Simba Wapewa MashartI/ Uchaguzi Wapamba Moto

Comments are closed.