Zahera Amtema Ajibu Dakika Za Mwisho Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongoman, Mwinyi Zahera amemuondoa dakika za mwisho nahodha na kiungo wake mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu kwenye msafara wa timu hiyo uliosafiri kwenda Iringa.

 

Timu hiyo, jana alfajiri ilianza sa­fari ya kwenda Iringa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakao­pigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Samora mkoani huko.

 

Ajibu amefikisha idadi ya wachezaji wanne iliyowaacha jijini Dar es Salaam kutokana na majeraha na adhabu ya kadi za njano, wengine ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Andrew Vicent ‘Dante’ na Juma Abdul.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Za­hera alisema mshambuliaji huyo ameon­dolewa baada

ya kupata majeraha ya nyonga wakiwa katika hatua ya mwisho ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Lipuli FC.

Zahera alisema alimtoa katika mipa­ngo yake ya mchezo na Lipuli baada ya kufanyiwa vipimo na daktari Mkuu wa timu hiyo, Edward Bavu na ku­gundulika ana maumivu ya majeraha hayo.

 

“Kama nilivyokueleza kawaida yangu, mimi katika timu sitegemei mchezaji mmoja, nina wachezaji wengi hata kama siku moja akikosekana mchezaji mmo­ja basi mwingine atachukua nafasi yake.

 

“Mfano mzuri, Ajibu nil­ishawahi kumuweka benchi katika baadhi ya michezo iliyopita ya ligi ukiwemo na Alliance na timu ikapata ushindi. Sina hofu kabisa, yupo Jaffary (Mo­hamed) aliye­tokea kwenye majeraha ya goti ambaye ninaamini ataweza kuziba vema nafasi yake,” alisema Zahera

Toa comment