The House of Favourite Newspapers

Zahera Amtuma Tambwe Aichinje Simba

 

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa anataka mshambuliaji wake, Amissi Tambwe aonyeshe uwezo wa juu kama alivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Singida United.

 

Zahera amesema anataka kumuona mshambuliaji huyo akiifungia timu yake mabao kwenye mchezo wa Jumapili.

 

Tambwe ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda kidogo, Jumapili iliyopita alifungia timu yake mabao mawili katika ushindi ambao Yanga iliupata wa mabao 2-0 katika Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji wake, Amissi Tambwe (wa pili kutoka kulia) akishangilia.

Kocha huyo alisema kuwa majukumu ambayo amekuwa akiwapa wachezaji wake wengi wamekuwa wakizingatia na atazidi kuwaelekeza pale ambapo wanakosea ili kuwa na kikosi imara zaidi.

 

“Tambwe kwenye mechi ile alifanya kile kitu ambacho nilimuomba kabla ya mechi kuhakikisha anacheza sana ndani ya mita 16 na kukimbia sana kuweza kupata bao jambo ambalo alifanikiwa kulifanya.

 

“Na kwa jinsi ambavyo alicheza siku ile ilionyesha wazi ana nafasi yake ndani ya timu kutokana na majukumu ambayo nilimpa aliyazingatia vizuri na kuweza kupambana, nimemwelekeza tena na naamini atafanya vizuri Jumapili,” alisema Zahera.

Comments are closed.