Zahera Ataja Kinachombakisha Yanga

Mwinyi Zahera, raia wa DR Congo.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, raia wa DR Congo ameweka wazi kuwa kitu pekee ambacho kinachomfanya aendelee kubaki kuifundisha Yanga hadi sasa ni kutokana na mdogo wake ambaye ndiye aliyemleta kwenye kikosi hicho.

 

Zahera hadi sasa ameiongoza Yanga katika michezo 18 ya Ligi Kuu
Bara na kuifanya timu hiyo kushika usukani wa ligi wakiwa na pointi 50 zikiwa ni pointi 10 mbele ya Azam FC wanaokamata nafasi ya pili, huku Simba ikiachwa pointi 17.

 

Kocha huyo amesema kwamba mdogo wake huyo ambaye anaishi Kenya, ndiye ambaye amekuwa akimwambia aendelee kubakia Yanga licha ya hali ngumu ya kiuchumi ambayo wanayo kwa sasa. “Ni mdogo wangu pekee anayeishi Kenya ndiye ambaye ananifanya niendelee
kubakia Yanga hadi leo hii kwa sababu yeye ndiye aliyechangia hadi mimi nimekuja hapa mwanzoni mwa msimu.

 

“Kabla ya kuja hapa, alishaniambia kila kitu juu ya Yanga hata hali hii ya matatizo ya kiuchumi lakini aliniambia haiwezi kuwa ya muda mrefu bali itaisha, lakini pia ninamsikiliza yeye kwa jinsi ambavyo ananiambia niendelee kukaa hapa ndiyo maana sijaondoka hadi leo licha ya changamoto ambazo tunapitia,” alisema Zahera.

STORI NA SAID ALLY

Loading...

Toa comment