The House of Favourite Newspapers

Zahera Ataja Mwisho wa Nyodo za Simba

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kama Simba akishinda viporo vyake vyote saba ndio anaweza kukata tamaa ya ubingwa msimu huu lakini kwa sasa anawaona kama wanapiga makelele tu. Zahera anasema kupoteza dhidi ya Lipuli siyo ishu sana kwa vile bado mapambano yanaendelea.

 

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 67 imecheza michezo 28, ikifuatiwa na Azam FC, wenye pointi 59 na michezo 28, wakati wapinzani wao Simba wakiwafukuza kwa mwendo kasi ambapo tayari wameshajikusanyia pointi 54 katika michezo 21 waliocheza hadi sasa.

 

Zahera ameliambia Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili kuwa; “Nitaanza kupoteza matumaini ya ubingwa baada ya kuiona Simba imeshinda viporo vyao vyote, kwani kama wakifanikiwa hivyo maana yake watakuwa wamekusanya pointi nyingi kuliko sisi au Azam, zaidi ya hapo sina shaka hata kidogo ya kuendelea kugombea ubingwa.”

 

“Kila mmoja anaijua changamoto yetu ya kiuchumi, hivyo hatujali sana hilo zaidi tunaangalia ubingwa ambao kwetu tukifanikiwa kuutwaa ninaimani utatufanya tupate hamasa kubwa ya kushiriki mashindano ya kimataifa tukiwa na nguvu nzuri.

 

“Mikakati iliyopo kwa sasa inaweza kufanikisha malengo mazuri ya usajili msimu ujao,” alisema Zahera ambaye ni Mkongomani mwenye uraia wa Ufaransa anayeishi Ufukwe wa Kawe Dar es Salaam.

 

KAGERE AMJIBU Meddie Kagere wa Simba amemjibu Zahera kwamba asitarajie wapoteze kwani wanajua hesabu zote zilivyo.

 

 

“Kitu pekee ambacho kitatupa fursa ya kuwa vinara ni ushindi hakuna jambo jingine ambalo tunatakiwa kufanya kwa sasa kwenye ligi, wapinzani wetu walipata matokeo na ndio maana wako pale walipo nasi njia yetu ni moja kushinda.

 

“Ushindani ni mkubwa na mara zote tumekuwa tukipambana na tunashukuru tunapata matokeo, kikubwa ni kutokata tamaa na mashabiki waendelee kutupa sapoti kuwa vinara ni suala la wakati tu,” alisema Kagere. Kagere ametupia mabao 13 kwa sasa akimuacha Heritier Makambo wa Yanga mwenye mabao 12.

MUSA MATEJA DAR ES SALAAM

Comments are closed.