Zahera hatari, ampoteza Aussems Bongo

Mbelgiji wa Simba, Patrick Aussems.

BAADA ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, kucheza mechi tatu nje ya Dar, timu hiyo imefanikiwa kuweka rekodi ya dakika 270 ambazo ni sawa na mechi hizo tatu, huku akimpoteza Mbelgiji wa Simba, Patrick Aussems.

 

Yanga kwa sasa imecheza jumla ya mechi 14, kati ya hizo, tatu pekee ndizo imecheza nje ya Dar ambapo ni Shinyanga, Kagera na Mbeya. Katika mechi hizo, imekusanya jumla ya pointi tisa.

Kocha Mwinyi Zahera raia wa DR Congo akiwa katika mazoezi na wachezaji wake.

Yanga ilianza kwa kuifunga Mwadui mabao 2-1 katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, kisha ikaibuka na ushindi kama huo mbele ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

 

Juzi Jumatatu, ikaibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Prisons, Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Hii inakuwa ni rekodi mpya kwa timu hiyo ndani ya msimu huu ikiwa chini ya kocha Mwinyi Zahera raia wa DR Congo licha ya awali kuelezwa timu hiyo isingeweza kufanya vizuri kwenye mechi za mikoani kutokana na kupita kwenye hali ngumu ya kiuchumi.

 

Kwa upande wa Simba ambayo ipo chini ya kocha Patrick Aussems, imecheza michezo minne mkoani ambapo walitoka sare na Ndanda ya Mtwara 0-0, ikifungwa na Mbao 1-0, ikashinda 3-1 dhidi ya Mwadui na ikashinda 2-0 dhidi ya JKT Tanzania.

 

Hivyo katika mechi hizo nne, Simba wameshinda mbili wametoka sare moja na kufungwa moja tofauti na Zahera ambaye kwenye tatu ameshinda zote.

Ibrahim Mussa,

Toa comment