The House of Favourite Newspapers

Zahera: Makambo Habari Nyingine, Atafunga Sana Tu

Straika wa Yanga, Heriti­er Makambo.

 

KOCHA Mkuu wa Yan­ga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amewe­ka wazi kwamba ana­muamini straika wake, Heriti­er Makambo kuwa ana uwezo wa kufunga zaidi ya mabao 16 kwenye ligi kutokana na kufunga idadi hiyo kwenye ligi ngumu ya Congo.

 

Makambo ana mabao saba sambamba na washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na Em­manuel Okwi .

Akizungumza na Championi Ijumaa, Zahera amesema kwamba anamuamini kwa saba­bu tayari alishafanya naye kazi nchini Congo na alifunga mabao mengi akipambana na timu kama TP Mazembe, hivyo hawezi kushindwa kufunga katika ligi ya Tanzania kutokana na kutoku­wepo ugumu sana kulinganisha na huko.

“Wakati ambao Makambo hakuwa anafunga mashabiki wakaanza kuongea lakini ni­waambie kwamba hilo suala siyo ishu kwake kwa sababu nime­fanya naye kazi DR Congo ali­wahi kufunga mabao 16 kwenye mechi nane za ligi.

“Kwenye suala la kufunga ninamuamini kwamba hatani­angusha na niwaambie kwamba atafunga zaidi, ni suala la ku­pewa muda tu,” alisema Zahera.

Stori na Said Ally,

Comments are closed.