Zahera: Tunaleta majembe mapya, mtatukoma

MKURUGENZI wa Ufundi wa Klabu ya Gwambina, Mkongomani, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa yupo kwenye mipango ya kukamilisha usajili wa nyota wa kimataifa hasa kisha wakapata suluhu dhidi ya Kagera Sugar, mchezo wa tatu wakapoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Zahera alisema washambuliaji ili kuongeza nguvu kikosi hicho ambacho kwenye michezo yao minne iliyopita hakijafunga bao lolote.

 

Gwambina ilitupa karata ya kwanza kwenye ligi dhidi ya Biashara United ambapo walipoteza kwa bao 1-0, kwenye michezo minne iliyopita timu hiyo ilikuwa ikicheza vizuri lakini tatizo kubwa limekuwa kwenye ufungaji.

 

“Tumekuwa na mwanzo mbaya kwenye michezo yetu minne ya Ligi Kuu Bara msimu huu, licha ya kuwa na kikosi kizuri lakini kupitia michezo hiyo minne tumegundua kuwa tuna upungufu kwenye eneo la ushambuliaji ambapo mpaka sasa hatujafanikiwa kufunga bao lolote.

 

“Kwa kulitambua hilo tumejipanga kufanya usajilli wa nyota kadhaa wa kimataifa hasa washambuliaji ili kuja kuongeza nguvu na ushindani kwenye kikosi,” alisema Zahera


Toa comment