The House of Favourite Newspapers

Zaidi ya 400 Wafariki Indonesia kwa Kimbunga cha Tsunami

An earthquake and a tsunami hit Palu on Sulawesi island

WATU wasiopungua 384 wamefariki dunia baada ya tetemeko la ardhi na kimbunga cha tsunami kuikumba Indonesia.

Habari kutoka jiji la Palu katika kisiwa cha Sulawesi zinasema mamia ya watu wamejeruhiwa na maelfu ya nyumba zimeharibiwa kutokana na dhoruba iliyosababishwa na mawimbi yaliyokuwa na urefu wa zaidi ya mita mbili.

Wengi wa waliofariki walikuwa katika ufukwe wa Palu, mji mkuu wa jimbo la Sulawesi Kati, ambapo ulifunikwa na taka na vifusi mbalimbali.Rescuers are struggling to reach the tsunami-hit areas

“Tsunami hiyo ilitokea jana, wakati watu walikuwa wakiendelea na shughuli zao ufukweni, na kwa vile ilikuja ghafla, hawakuweza kukimbia,” alisema ofisa mmoja anayeshughulikia majanga, Sutopo Purwo Nugroho.

Residents examine the tsunami aftermath in Palu

Mamlaka za serikali zinafanya juhudi za kurudisha huduma mbalimbali eneo hilo ikiwa ni pamoja na umeme na kukabiliana na mamia ya majeruhi wanaohitaji tiba.

 

Medical team members help patients outside a hospital after an earthquake and a tsunami hit PaluWafanyakazi wa tiba wakiwasaidia majeruhi nje ya hospitali moja huko  Palu

Comments are closed.