
Benki ya NMB imepanga kutumia zaidi ya Sh.120 bilioni kutoa mikopo ya mitaji, vifaa na mitambo kwa wachimbaji
wadogo wa madini kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza tija katika Sekta ya Madini nchini. Akizungumza
jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Klabu la Wachimba Madini Kanda ya ziwa, (NMB Mining Club) Mkuu wa Idara
ya Biashara wa NMB, Alex Mgeni alisema hadi sasa, tayari benki hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya
Sh.63 bilioni kwa kundi hilo.
“Wachimbaji wadogo watakopeshwa vifaa na mitambo bila kulazimika kuweka dhamana kwa sababu mitambo na
vifaa hivyo ndivyo vutakuwa dhamana yao baada ya kulipa kuanzia asilimia 20 ya thamani ya kifaa au mtambo
anaotaka kununua,” alisema Mgeni.
Akizuzugumza wakati wa hafla hiyo iliyoshirikisha wachimbaji zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu,
Geita, Shinyanga na Kagera, Rais wa Shirikisho la Wachimba Madini Tanzania (Femata), John Bina alisema uamuzi
wa benki ya NMB kuanzisha dirisha la mikopo kwa Sekta ya Madini siyo tu utaongeza tija, bali pia utakuza uchumi
wa wachimbaji na Taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel aliihakikishia NMB utayari wa Serikali wa kushirikiana na taasisi za
fedha na wadau wengine kutekeleza sera na mikakati ya kuongeza tija katika sekta ya madini aliyosema imekuwa
kwa kasi ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Aliwashauri wachimbaji wadogo nchini kuunganisha nguvu kimtaji kumudu siyo tu kufungua migodi ya kati na
mikubwa, bali pia kutoa huduma katika migodi mikubwa ya Kimataifa kupitia sera ya local content inayoelekeza
sehemu ya huduma migodini kutolewa na kampuni za wazawa.

Kuhusu “NMB Mining Club ni mpango unaolenga kufikia miji sita nchini yaani Mwanza, Chunya, Morogoro na Arusha, ulianzia
Dodoma na Kahama na maeneo ya karibu kwa lengo la uwezeshaji na kutoa mafunzo ya biashara, elimu ya mwendelezo wa
kitaalamu wa madini) na fursa ya kukutana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.. Ubunifu huu ndio unaoifanya NMB
kuendelea kuwa kinara wa huduma na bidhaa katika sekta ya kibenki

