The House of Favourite Newspapers

Zaidi ya Wanafunzi 70 Wanusurika Kifo Baada ya Bweni Lao Kuteketea kwa Moto

0
Mali za wanafunzi zimeteketea vibaya katika ajali hiyo ya moto

ZAIDI ya wanafunzi 70 katika shule ya wavulana ya Bwiru Sekondari iliyopo manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wamenusurika kifo baada ya bweni kuteketea kwa moto.

Wanafunzi wakiwa nje wakishuhudia Bweni lao likiteketea kwa moto

Tukio hilo limetokea majira ya saa 3:40 usiku wa kuamkia leo wakati wakiwa madarasani wakijisomea masomo yao ya ziada.

Miundombinu ya Shule hiyo ikiwa imeharibiwa na ajali ya moto

Tayari Mamlaka husika zinaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha tatizo ingawa madhara ni makubwa ikiwemo kuteketea kwa mali za wanafunzi pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya shule.

Leave A Reply