ZAMARADI AELEZA SABABU ZA KUMCHANGIA RUGE

Zamaradi Mketema ‘Zama’

UBINADAMU kwanza! Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha filamu cha Take-One kilichokuwa kikirushwa na Televisheni Clouds, Zamaradi Mketema ‘Zama’ ambaye pia ni mzazi mwenza wa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameeleza sababu ya kuhamasisha watu wamchangie jamaa huyo fedha za matibabu.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Zamaradi alisema kuwa angeonekana mtu wa ajabu na watu wangejiuliza endapo na yeye angekuwa nyuma kutohamasisha watu kuchangia matibabu ya Ruge ambaye pia ni baba wa watoto wake wawili. “Unajua watu wangekuwa kwenye mshangao endapo nisingefanya kitendo cha uungwana cha kuamua na mimi kuchangisha.

 

“Hata mume wangu angenishangaa, lakini pia ugonjwa siyo kitu cha kufanya mashindano hata kidogo maana yeyote anaweza kuumwa,” alisema Zamaradi. Kingine mtangazaji huyo alisema kuwa watu wakumbuke kuwa anaishi na watoto ambao ni damu ya Ruge, kwa hiyo kama angejiweka pembeni, watoto wake wasingemwelewa kwa sababu ni baba yao hata iweje.

“Watoto wangu wanampenda baba yao na wanampenda baba anayewalea hivi sasa, lakini mimi kutoonesha kuguswa katika hili, hata watoto wangu wangenishangaa sana. “Unajua suala la mgonjwa linamgusa kila mtu,” alisema Zamaradi ambaye ameweka maelezo kwenye ukurasa wake wa Instagram akihamashisha watu kujitokeza kumchangia Ruge fedha za matibabu.

 

Ruge alianza kuchangiwa fedha za matibabu mwanzoni mwa wiki hii baada ya familia yake kuomba kusaidiwa katika kipindi hiki ambacho jamaa huyo anaendelea na matibabu ya matatizo ya figo nchini Afrika Kusini.

 

Zama alitengana na Ruge mwaka juzi baada ya kuishi wote kwa miaka kadhaa kama mume na mke ambapo katika uhusiano wao walijaliwa watoto wawili. Baada ya kutemana na Ruge, Zama aliolewa rasmi kwa ndoa ambayo anaitumikia hadi leo

Loading...

Toa comment