The House of Favourite Newspapers

Zamaradi Kuwakutanisha Mastaa Sabasaba

0

MTANGAZAJI maarufu ambaye anamiliki Zamaradi TV, Zamaradi Mketema anatarajia kuwakutanisha mastaa mbalimbali Bongo ambao ni wafanyabiashara ndani ya maonyesho ya Sabasaba kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Zamaradi alisema kuwa, ameamua kufanya hivyo kwa mastaa mbalimbali kwa sababu kuna mashabiki wengi wanapenda sana kununua vitu kutoka kwao lakini wengine hawajui wanapatikana wapi hivyo ni njia rahisi ya wao kujitangaza.

“Unajua wengi wanatamani hata kuzungumza na mastaa wetu idea mbalimbali lakini hawana uwezo wa kuwaona sasa nimeona jambo zuri kuwakutanisha wote Sabasaba ndani ya banda moja ambapo watakuwepo Wema Sepetu, Kajala Masanja, Aunt Ezekiel, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, wanawake wa tasnia ya filamu wote na watu watapata fursa ya kupiga nao picha,” alisema Zamaradi.

Leave A Reply