The House of Favourite Newspapers

Zanzibar Kuwa Mwenyeji Tuzo za Muziki za Trace 2025 kwa Udhamini wa Johnnie Walker


Dar es Salaam, Tanzania – Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) inayo furaha kutangaza kuwa Zanzibar itakuwa mwenyeji wa Tuzo za Muziki za Trace 2025, tukio kubwa litakalodhaminiwa na kinywaji cha Johnnie Walker kama mdhamini mkuu.

Tukio hili linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24 hadi 26 mwezi Februari katika hoteli ya kifahari ya
Mora Resort, visiwani Zanzibar nchini Tanzania, linalenga kusherehekea mabadiliko ya muziki
na utamaduni wa Kiafrika—sehemu muhimu ya urithi wa kisanaa wa Tanzania na faida yake
inayoongezeka kimataifa.


Tuzo za Trace na Mkutano wa 2025 utatambua vipaji vya muziki wa Afrika katika vipengele 24
tofauti, ambapo Johnnie Walker itadhamini tuzo mbili kuu: Wimbo Bora wa Mwaka na Msanii
Bora Chipukizi. Tukio hili pia litajumuisha mkutano wa siku mbili ambao utakuwa na mijadala ya
kibunifu, mafunzo, na majadiliano kuhusu maendeleo ya tasnia ya muziki, teknolojia, na uimarishaji wa chapa barani Afrika. Washiriki watajumuisha wasanii, mameneja, ma-DJ, maprodyuza, na wadau wengine wa sekta hii kutoka ndani na nje ya Afrika.


Mwaka huu, ushirikiano huu kati ya Johnnie Walker na Tuzo za Muziki za Trace unasisitiza
dhamira ya Johnnie Walker ya kusherehekea utamaduni wa Kiafrika na kuchochea mijadala
yenye tija.

Kama moja ya majukwaa yanayoheshimika zaidi kwa muziki wa Kiafrika na Afro-
urban, Tuzo za Trace zinatambua vipaji na uvumbuzi kwa kiwango cha kimataifa, zikitanguliza
ubunifu, utamaduni, na maendeleo— zikiakisi kaulimbiu ya Johnnie Walker ya ‘Keep Walking’,
ambayo inahamasisha maendeleo, ubunifu, na kwenda mbali zaidi.


Akizungumzia ushirikiano huu, Henry Esiaba, Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu wa SBL, alisisitiza umuhimu wa tukio hili kwa Tanzania na chapa ya Johnnie Walker akisema, “Tunajivunia kuwa na Johnnie Walker kama mdhamini mkuu wa Tuzo za Muziki za Trace 2025 na kuona Tanzania ikiandaa tukio hili linalotambulika kimataifa.

Ushirikiano huu hauitangazi tu  Tanzania kimataifa bali pia inaashiria kaulimbiu ya ‘Keep Walking’-kuadhimisha maendeleo na kuhamasisha vizazi vijavyo.”
Naye, Irene Mutiganzi, Mkuu wa Kitengo cha Vinywaji Vikali-Masoko kutoka SBL alisema, “Tuzo
za Muziki za Trace 2025 ni zaidi ya sherehe ya muziki—ni sherehe ya maendeleo, ubunifu, na
uthubutu.

Kwa Johnnie Walker, ushirikiano huu ni ishara kubwa ya dhamira yetu ya kuwa bega
kwa bega na wabunifu na wavumbuzi wanaotengeneza mustakabali wa kesho. Tunatazamia
kuonesha ubora wa muziki na utamaduni wa Kiafrika kwa ulimwengu mzima.”
Katika kipindi cha kuelekea kwenye tukio hili, sehemu nyingine muhimu ya hafla hii itakuwa
Ziara ya Tuzo za Trace, ambayo itatembelea miji mikubwa ya Afrika, ikiwemo Tanzania. Ziara hii
itajumuisha maonesho ya moja kwa moja ya muziki na fursa za mashabiki kukutana na wasanii

walioteuliwa. Kwa Tanzania, tukio hili litafanyika tarehe 7 mwezi Februari 2025 na litakuwa
utangulizi wa tukio kuu la utoaji wa tuzo.
Kama mwenyeji, Tanzania itang’ara kama kitovu cha ubunifu, utamaduni, na ukarimu. Zanzibar,
yenye mandhari ya kuvutia na urithi wake mkubwa, inatoa mazingira bora kwa tuzo hizi.
Ushirikiano huu pia unathibitisha dhamira ya SBL ya kusaidia mipango inayoinua hadhi ya taifa
na kusherehekea utajiri wake wa kitamaduni.
Kupitia ushirikiano huu, Johnnie Walker na Trace wataandaa burudani kubwa na ya kipekee
wakati wa Tuzo za Trace, ikiwapa wageni burudani inayoendana na chapa ya Johnnie Walker
huku wakisherehekea mvuto wa utamaduni wa Afrika.