The House of Favourite Newspapers

Kiroho Safi, Zari Amfariji Mobeto

DAR ES SALAAM: Kwa mara ya kwanza, mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amevunja ukimya na kuamua kumfariji ‘mke mwenzake’ Hamisa Mobeto baada ya watu kumshambulia mitandaoni.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, jana Zari aliweka ujumbe ulioshiria kumfariji Mobeto bila kumtaja jina na ndipo watu walipojiongeza kwa kusema, amemfariji mrembo huyo kutokana na sakata lake la kuvuja kwa sauti iliyosikika akizungumza na mganga ili amroge mzazi mwenzake Diamond.

 

“Usiwape nguvu watu ya kukulinganisha wewe na watu wengine, kama hawawezi kuamua, waamulie, songa mbele na usigeuke nyuma, nenda mahali kwenye furaha, hakuna sababu ya kumuelezea kila mtu kwani safari ni yako, hakuna anayeelewa zaidi yako, hakuna cha kupeleka zaidi ya upendo kwa dada yangu wa Tanzania, futa machozi na hilo lipite,” aliandika Zari kwa lugha ya kingereza.

Risasi Jumamosi lilimvutia waya Zari ambapo alipopatikana alithibitisha kuwa ujumbe huo alimtumia Mobeto na kusema amefanya hivyo kiroho safi.

“Tunapaswa kusambaza upendo kwa sababu baadhi ya watu wanahitaji kutiwa moyo,” alisema Zari.

 

Wawili hao kwa nyakati tofauti wamezaa na staa wa Bongo Fleva, Diamond. Zari amezaa naye watoto wawili na kuachana naye huku Mobeto akizaa naye mtoto mmoja, ambapo pia wamemwagana.

STORI: Memorise Richard, Risasi Jumamosi.

Comments are closed.