The House of Favourite Newspapers

ZARI AJILIPUA KAMA MOBETO

IMEFICHUKA! Alichokifanya zilipendwa wa mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (30), Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ (40) kimeendelea kuzua mjadala huku kikitafsiriwa kuwa ni kujilipua kama ilivyokuwa kwa zilipendwa mwingine kwa jamaa huyo, Hamisa Mobeto ‘Tununu’ (25).

 

Miezi kadhaa iliyopita, Mobeto ambaye ni mama wa watoto wawili alijilipua kwa kudaiwa kujiweka kimapenzi kwa mwanaume aliyetajwa kwa jina la Josh Adeyeye (25) walipokuwa nchini Marekani.

Hata hivyo, katika nusanusa ya wadaku, yaliibuka mambo mengi likiwemo suala la Mobeto kufanya hivyo ili kumrusha roho Diamond au Mondi ambaye alikuwa amempiga kando baada ya kuzaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Dyllan.

 

Mwisho wa yote, pamoja na kumrusha roho Mondi, lakini Mobeto alidaiwa kutumia fursa hiyo kufanya ‘kiki’ ya wimbo wake mpya wa Tunaendana ambapo ndani ya video yake anaonekana akiwa kimahaba na jamaa huyo.

Baada ya ‘project’ hiyo, Mobeto alirejea nyumbani na kuwa kimya kabla ya hivi karibuni kudaiwa kukwapua bwana wa mtu na kwenda kula naye bata visiwani Zanzibar kisha kudaiwa kufumaniwa naye.

ZARI KAMA MOBETO

Kama ilivyokuwa kwa Mobeto, mara baada ya Siku ya Valentine iliyochukua nafasi wiki iliyopita, Zari naye aliibuka na mwanaume mpya na kuzua mjadala mzito. Tofauti na alivyoeleza awali kuwa baada ya kutengana na Mondi hawezi kumtangaza mwanaume wake mpya kwani ni wa kwake na siyo wa mitandaoni, Zari alimwanika mwanaume huyo nusunusu mitandaoni bila kumuonesha sura.

 

Hata hivyo, wafuatiliaji wa mambo ya watu walisaka wasifu wa jamaa huyo na kuuanika kuwa jina lake ni Danny na ni modo anayefanyia kazi zake nchini Afrika Kusini akiwa na asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Pamoja na hayo ilielezwa kuwa jamaa huyo ana mkwanja mrefu na kuthibitisha ile kauli ya mwanamama huyo ambaye aliwahi kukaririwa akisema kuwa hajawahi kuwa kwenye uhusiano na mwanaume choka mbaya asiyekuwa na mkwanja zaidi ya Mondi ambaye alimpenda kwa dhati bila kujali kama ana pesa.

TEAM ZARI WARUSHA MADONGO

Kufuatia uamuzi huo wa Zari kumwanika mwanaume huyo kupitia Mtandao wa Snapchat, wafuasi wake wanaojiita Team Zari walijikuta wakirusha madongo mitandaoni wakimsifia mwanaume huyo kuwa ni handsome ukilinganisha na Mondi.

“Mwacheni Mama Tee ainjoi maisha, huyo Dai (Mondi) ajue malipo ni hapahapa dunia maana alidhani Zari hatapata mwanaume? “Sasa kifaa ndiyo hicho hapo, mwanaume wa ukweli. “Alikuwa anamsubiri tu huyo Baba Tee (Mondi) amtangaze mwanamke wake mpya (Tanasha) ndiyo na yeye (Zari) aibuke na kifaa chake.

“Sasa hivi tunaweza kusema ngoma ni droo, lakini Diamond amechezea wanawake sana, ngoja na yeye aumizwe roho maana tunajua yupo na Tanasha, lakini bado anampenda sana Zari. “Yaani natamani kesho Tiffah (mtoto mkubwa wa Mondi) apelekwe kwenye mbuga za wanyama na baba wa kambo ili Diamond afundishwe kuwa baba bora, najua soon Zari atafanya hivyo maana dozi zake huwa ni kiboko.

“Unajua Zari kwa muda mrefu hakutaka kumuonesha Diamond kuwa kuna wanaume wa maana wanamtaka kwa sababu aliamini Diamond angejirudi halafu waendelee na maisha, lakini baada ya kumuona jamaa akitamba na Tanasha ndipo naye akasema liwalo na liwe,” zilisomeka baadhi ya komenti nyingi kwenye mitandao ya kijamii juu ya Zari kumpata bwana huyo mpya.

TULIKOTOKA

Zari aliyejaliwa watoto wawili na Mondi, alitengana na jamaa huyo yapata mwaka mmoja uliopita kutokana na kile alichokieleza mwanamama huyo kuwa mwanaume huyo alimvunjia heshima kwa kumsaliti na wanawake wengine.

Comments are closed.