Zari Ajivunia Kuwaleta Watoto Bongo

ROHO ya mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, sasa ni kwatu baada ya kufanikisha zoezi la kuwaleta wanawe, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ na Nillan Nasibu ‘Prince Nillan’ kwa baba yao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Taarifa ikufikie kwamba, Zari anajivunia mno kufanikisha kuwaleta watoto hao Bongo na kwamba zoezi hilo limewaweka watu kwenye mstari ulionyooka.

Zari anasema kuwa, ishu hiyo imewanyamazisha wengi kwani kwa sasa hali siyo kama zamani.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA kwa njia ya simu baada ya kurejea maskani kwake, Durban nchini Afrika Kusini akiwa na wanawe hao, Zari anasema kuwa, alipopanga safari ya kutinga Bongo hakujua kwamba baadhi ya watu watakuwa hawali wala hawalali kwa ajili yake.

Zari anasema kuwa, ameona wazi siku chache alizokaa Bongo, kila mtu amekaa kwenye mstari wake ulionyooka na manenomaneno waliokuwa wanayaongea wafitini wake, hayapo tena.

 

“Kuja huko (Bongo) kidogo tu, watu wote wametulia kimya, hakuna wa kusema jambo lolote kama wanavyosemaga kwenye mitandao ya kijamii, sasa ningekaa mwezi, sijui ingekuwaje kwa kweli,” anasema Zari ambaye amezaa watoto wawili na Mondi.

Zari ambaye ni mjasiriamali, raia wa Uganda aliwasili Bongo wiki mbili zilizopita akiwaleta watoto hao baba yao.

 

Alisema kuwa, alifanya hivyo baada ya kuwepo kwa maneno mengi mitandaoni.

“Kuna maneno mengi yanaendelea kwenye mitandao, wengine wakisema nimekuja kurudiana na Diamond, lakini wanashindwa kufahamu kwamba mimi nimewaleta watoto wangu kuja kumuona baba yao baada ya kuachana kwa muda mrefu,” alisema Zari.

Aliongeza kuwa, Tanzania ni kama nyumbani kwake ana uwezo wa kuja kuishi ingawa hilo haliondoi kwamba yeye na Mondi ni wazazi wa watoto wawili, lazima wakati fulani watashirikiana tu.

 

Stori: Imelda Mtema

Toa comment