Zari Ammisi Diamond Platnumz

BAADA ya kuachana na bwana’ke mwingine aliyepewa jina la Dark Stallion (Farasi Mweusi), baby mama wa staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz, Zarinah Hassan au Zari The Boss Lady amesababisha sintofahamu, IJUMAA limedokezwa.

 

Mwanamama Zari ambaye ni raia wa Uganda mwenye maskani yake, Durban nchini Afrika Kusini, amesababisha mjadala mpya kutoka kwa wafuasi wake almaarufu Team Zari kwamba ni rasmi sasa amerejesha majeshi kwa mwamba Diamond.

 

ZARI AMEMMISI MONDI?

Team Zari wanadai kwamba, Zari amesababisha mshangao kwao baada ya kudaiwa kummisi Diamond au Mondi; muda mfupi baada ya kumwagana na huyo Dark Stallion ambaye jina lake halisi ni Frederick Nuamah, mwigizaji na prodyuza mkubwa wa filamu nchini Ghana.Zari ambaye ni mama wa watoto watano, anasema kuwa, anammisi mtu f’lani ambaye Team Zari wanadai si mwingine, bali ni Mondi.

TIFFAH ATHIBITISHA

Madai hayo ya Team Zari yanathibitishwa na binti yake ambaye Zari amezaa na Mondi, Latifah Nasibu almaarufu Tiffah Dangote ambaye amebumburua sii nzito baada ya kudai mwanamama huyo yupo kwenye mapenzi na baba yake ambaye ni Mondi.

 

Tiffah Dangote au Princess Tiffah anasema mama yake amekufa na kuoza kwenye mapenzi ya baba yake, Mondi; na jambo hilo amelisema ‘live’ akirekodiwa na mama yake huyo.Tiffah Dangote alibumburua hayo alipokuwa akizungumza na wafuasi wake zaidi ya milioni 2.8 kwenye Instagram ndipo alipojikuta akitamka yale yaliyoujaza moyo wake kwamba, mama yake, Zari na Mondi wapo kwenye mapenzi kwa mara nyingine.

 

ZARI APATA MSHTUKO

Kutokana na mshtuko alioupata kwa kauli ya Tiffah Dangote, Zari alilazimika kumnyamazisha kwa haraka katikati ya sentensi akionesha kwamba alikuwa anaendelea kuelezea uhusiano huo wa mama na baba yake, lakini tayari dunia ilikuwa imeshadaka maneno hayo kwamba; ‘mama yupo kwenye mapenzi na baba’!

 

KWA MUDA MREFU

Kwa muda mrefu sasa, Zari amekuwa akihisiwa kurejesha majeshi kwa Mondi na sasa baada ya kumwagana na Dark Stallion, wawili hao wana kipindi chao cha televisheni kinachotarajiwa kuanza kuruka hewani kupitia mtandao mkubwa wa sinema duniani wa Netflix.Kwa mujibu wa Zari, katika uhusiano aliokuwa nao wa Dark Stallion haukumjenga.Zari anasema; “Kama uhusiano haukunijenga, nisiingeendelea nao…

 

Kwa mujibu wa watu wa karibu, kinachoonekana ni kwamba, Zari ameamua kumwacha mwanaume huyo aende kwa sababu bado anampenda Mondi.Imeelezwa kwamba, ni jambo ambalo lipo wazi kwani, haiwezekani mtu aliyeachana naye tangu Februari 14, 2018, lakini bado anaendelea kumuwaza na kumzungumzia kama si kweli kwamba bado anampenda.

 

MAONI YA TEAM ZARI

Juu ya kauli ya Tiffah, Team Zario wamekuwa na maoni tofauti;“Watoto ni wakweli siku zote juu ya kile wanachokijua.“Watoto na walevi kamwe hawadanganyi, hawa watu (Zari na Mondi) kuna kitu.“Tiffah ametumwa na mama yake. Huyu Zari bado anammisi Diamond.

 

“Watoto ni malaika, hawasemi kitu wasichokijua.“Warudiane tu kwa sababu muda mwingi Diamond anautumia kwa Zari na watoto wao kuliko wanawake na watoto wake wengine, bora uhai acha sisi tulio singo tusubiri muda wetu.“Tiffah anaipenda Tanzania ndiyo maana kila mara hawezi kukaa bila kuitaja na kuiombea.“Tiffah anapenda kuwaona wazazi wake pamoja.“Diamond hampendi mwingine zaidi ya Zari.“Kwa Mungu kila kitu kinawezekana.

 

“Nadhani hii ni gia ya Zari kumsahau Dark Stallion na kurejea kwa Diamond.“Kicheko cha Tiffah ni cha kweli, anasema ukweli wa kile anachokijua juu ya wazazi wake, kamwe watoto hawasemi uongo.“Tiffah amechoma kibanda.“Zari ameamua kumtumia Tiffah kufikisha ujumbe kwa sababu Diamond anamsikiliza sana Tiffah na anampenda mno…“Kumbe ndiyo maana Dark Stallion ameachwa.“Zari akirudiana na Diamond haina shida, acha warudiane…” Ilisomeka sehemu ya maoni lukuki juu ya video hiyo ya Tiffah.

 

ZARI NA MONDI MAJIMBO YAPO WAZI

Kabla ya kuruka kimapenzi na Mondi, Zari alikuwa mke wa ndoa wa marehemu Ivan Semwanga ambaye alikuwa mfanyabiashara tajiri wa Uganda ambaye alizaa naye watoto watatu kabla ya kukutwa na umauti mwaka 2017.Baada ya hapo, Zari akawa na Mondi ambaye amezaa naye watoto wawili ambao ni Tiffah Dangote na Prince Nillan kabla ya kumwagana mwaka 2018.

 

Baada ya hapo, Zari alidaiwa kuwa kwenye mapenzi na jamaa mwingine aliyemtambulisha kama King Bae kabla ya kutua kwa Dark Stallion ambaye naye wameachana hivyo kudaiwa kurejesha majeshi kwa Mondi.Kwa upande wake, Mondi baada ya kutengana na Zari alitoka kimapenzi na mwanamitindo Hamisa Mobeto ambaye alizaa naye mtoto mmoja wa kiume na Tanasha Donna ambaye naye amezaa mtoto mmoja wa kiume na sasa yupo singo hivyo wote majimbo yapo wazi.


Toa comment