The House of Favourite Newspapers

ZARI AMWEKEA DIAMOND MWANASHERIA

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’

MFANYABIASHARA Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amedaiwa kumwekea mzazi mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwanasheria kwa ajili ya kumsimamia ili awalee watoto wake katika misingi bora licha ya kuwa wameshatengana.

Chanzo kilicho karibu na wazazi hao kimeeleza kuwa, Zari ni mwanamke ambaye yuko ‘siriaz’ na malezi ya watoto hivyo ameamua kumwekea mzazi mwenzake huyo mwanasheria ili aweze kuwajibika kwa asilimia mia moja bila kukosa hata jambo moja la msingi.

“Unaambia siri ya Diamond kwenda Sauz (Afrika Kusini) kila mwezi ni baada ya kuwekewa mwanasheria huyo ambaye anamfuatilia kwa karibu ili kuhakikisha haendi kinyume na matakwa ya sheria,” kilisema chanzo hicho. Aidha, chanzo hicho kilidai kuwa, Diamond wikiendi iliyopita alikuwa Sauz ambapo alionekana yuko karibu na watoto wake na kuwapa mahitaji yote muhimu.

“Unajua hata akiwa na shoo vipi ameambiwa ajipange ili kutofautiana na ratiba za watoto na akifika nyumbani pale kwa Zari wanalala chumba tofauti ingawa siku nyingine anakwenda kulala hotelini,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika. Baada ya ubuyu huo kutua gazetini, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond ambapo alipopatikana alikiri kuwa yupo Sauz na kudai kuwa amezoea watu kuongea mambo ya watu hivyo hatawajali.

“Waswahili nimewazoea sana tu, wasiponiongelea na Zari hawaoni sawa, mimi huwa nakuja huku kwa ajili ya kuwaona watoto wangu, natimiza majukumu kama baba, hayo mengine nawaachia wao,” alisema Diamond. Februari mwaka huu, Zari ambaye amemzalia watoto wawili Diamond, aliutangazia umma kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa ameamua kuachana na mzazi mwenzake huyo kutokana na kumshindwa tabia.

STORI: Imelda Mtema, DAR

Comments are closed.