The House of Favourite Newspapers
gunners X

Zari Ateswa na Watoto

0

ANATESEKA! Ndiyo lugha rahisi inayoweza kutafsiri kile anachopitia mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kufuatia kuonekana kuzidiwa na gharama za watoto wake wakiwemo wawili aliozaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Mondi’.

Iko hivi; Serikali ya Afrika Kusini anakoishi Zari, imefunga shule zote na kuzuia mikusanyiko hadi Aprili 14, mwaka huu ili kujilinda na maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha Ugonjwa wa COVID-19.

Serikali hiyo baada ya kufunga shule, ikaweka utaratibu wa wanafunzi kusoma kwa njia ya mtandao katika kipindi hicho cha mpito.

Kitendo cha Serikali kutangaza kufunga shule hizo, Zari akatoa povu kama lote kuonesha kwamba hakubaliani na mpango wa Serikali, jambo ambalo limetafsiriwa kuwa anateseka na gharama.

Zari alisema, anaiomba Serikali iangalie upya kuhusu suala hilo maana si wazazi wote wanaweza kumudu kuwasomesha watoto wao kwa njia hiyo ya mtandao.

“Lazima watambue kwamba kuna watu wenye uwezo na wasio na uwezo na wote wana haki ya kupata elimu,” alilalamika Zari.

Wachambuzi wa kwenye mitandao, ndipo walipojiongeza na kumsema Zari kuwa hana lolote, anateswa na gharama za kusomesha.

“Mh! Bibie aseme tu asaidiwe, maana haiwezekani Serikali itoe tahadhari kama hii halafu umewekwa mpango mzuri kama huu, yeye ashindwe kugharamia,” alisema mdau mmoja mtandaoni.

Wengine walikwenda mbali zaidi kwa kumwambia kama anaona watoto hao wa Mondi; Tiffah na Nillan wanamshinda kuwagharamia, angewarudisha kwa baba yao, kwani hajawahi kusema kwamba anashindwa kuwalea.

Zari na Mondi waliachana Februari 14, mwaka jana ambapo watoto waliowapata kwenye uhusiano wao, walibaki na bibie huyo Sauz huku Mondi akionekana kutopewa nafasi ya kwenda kuwaona hadi ulipoibuka ugonjwa wa Covid-19 ulioanzia huko nchini China.

Hadi mwishoni mwa wiki iliyopita, Afrika Kusini ilikuwa imerekodi waathirika 116 walioambukizwa virusi vya Corona.

Leave A Reply