The House of Favourite Newspapers

Zari, Diamond biashara imekwisha!

0

diamondplatnumznazarir.jpg Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Mwandishi wetu
BIASHARA imekwisha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia ‘kapo’ ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kudaiwa kuwa waliweka misingi ya penzi zito ili Diamond apate mtoto hivyo baada ya mrembo huyo kujifungua Latifah ‘Tiffah’ miezi miwili iliyopita, penzi halitakuwa motomoto kama zamani, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.
Chanzo cha uhakika kilicho karibu na wawili hao, kimesema makubaliano ya awali baina ya wazazi hao, yalikuwa ni kwa mwanamke huyo raia wa Uganda, kumzalia mtoto Diamond ambaye alikuwa akisaka ubaba kwa udi na uvumba.

TIFFAH DIAMOND (4)TUJIUNGE NA CHANZO
“Wote mnajua jinsi Diamond alivyokuwa akihangaika kupata mtoto, maana wapenzi wake wote wa awali hawakuweza kumzalia. Sasa alipokutana na Zari ambaye tayari alikuwa na watoto, wakakubaliana kwa masharti kuwa ndani ya muda f’lani, amzalie.

“Sasa ndiyo ikawa hivyo, baada ya Tiffah kuzaliwa, kila mtu sasa yupo huru kufanya yake, ndiyo maana Zari amerudi kwake Afrika Kusini ‘Sauz’ na hawezi kuja kuendelea kuishi na Diamond kama wakati ule wa ujauzito.
“Kule Sauz, Zari anaendelea na biashara zake na nimesikia kwa sasa anaandaa Zari All White Party kama ile aliyoifanya Mlimani City hapa Bongo,” kilisema chanzo chetu.

ZARINADIAMOND4KWA NINI HAWEZI KURUDI?

Chanzo hicho kiliendelea kutoboa siri kwamba, pamoja na makubaliano ya kuzaa, lakini pia mazingira ya sasa ya makazi ya Diamond hayatoi nafasi kwa mwanamke huyo mwenye fedha ambaye pia ni msanii, kuweza kuishi.
“Sasa hivi pale nyumbani kwa Diamond kumejaa, imekuwa familia kubwa. Maana kuna mjomba wake Diamond anaishi pale, dada zake wawili, Esma na Queen Darleen wanaishi pale. Mama yake Diamond (Sanura Kasim) yupo pale.
“Haya, achana na ndugu wengine. Lakini pia kuna wasichana wa kazi wawili na mlinzi mmoja. Sasa kwa mtu kama Zari ambaye maisha yake ni ya kisupastaa hawezi kuishi kwenye nyumba yenye watu wengi hivyo.”

ZARI ANAOGOPA UMBEYA
“Pia inasemekana Zari hataki kuishi na wifi zake kwa sababu anaogopa umbeya. Hata wakati ule alipokuwa mjamzito mpaka kujifungua, hakuwa mtu wa kujichanganya nao sana. Alikuwa mtu wa peke yake peke yake tu.”

HAKUNA TENA MAPENZI?
“Taarifa nilizonazo ni kuwa, Diamond na Zari watakuwa wanaendelea na uhusiano wao wa kimapenzi lakini si ule wa kama awali. Ila wataendelea kuwa watu waliozaa mtoto na maisha ya Tiffah yataendelea kuwa kwa mama yake hadi hapo watakapoamua vinginevyo. Zari anaweza kuja Bongo na Diamond anaweza kwenda Sauz kwa Zari.”
“Zari hataki kuishi Tanzania, anataka Tiffah aishi na ndugu zake kule Sauz hadi akue na kuanza masomo. Kwa hiyo usitegemee ule ukaribu kama wa mwanzo.”

KUHUSU DIAMOND!
Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba ikielezwa kuwa yupo nchini Marekani katika shughuli za kimuziki. Hata alipotumiwa meseji kwa njia ya Mtandao wa WhatsApp hakujibu.
Hata hivyo, mtu wake wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alitatizwa na suala hili akisema:
“Dah! Wabongo bwana! Ninachojua mimi ni kuwa, bado watakuwa wapenzi japokuwa siwasemei maana Diamond naye haaminiki sana. Si unajua ameshapata mtoto, lolote linaweza kutokea.
“Ila Diamond akimhitaji Zari aje Tanzania anaweza kuja, akitaka aende Sauz atakwenda kwa sababu Tiffah lazima alelewe na wazazi wote.
“Halafu lazima ujue kwamba, Zari ni mfanyabiashara, ana biashara zake Afrika Kusini na Uganda. Kwa hiyo siyo mtu ambaye unaweza kumtegemea akae sehemu moja tu.”

Leave A Reply