Zari minyoosho kama yote!

WAKATI upande wa pili huku wakiwa bize na mambo yao ya kusubiri mtoto na nini na nini, huko Sauz mambo ni moto kwani aliyekuwa mpenzi wa Mondi, Zari naye amezidi kutupia picha za kimalovee akiwa na mwanaume anayedai kuwa ni mumewe. Kupitia kipengele cha Insta Story, Zari alitupia picha yenye kivuli cha kiaina ikimuonesha akiwa na jamaa wake wakibusiana midomo yao kitendo ambacho kiliwafanya baadhi ya mashabiki washushe povu.

“Mh! Huyu naye si atulie watu tuko bize huku tunasubiria kichanga yeye anatuonesha malovee sisi inahusu?” alichangia mdau mmoja huko Instagram na kuungwa mkono na wenzake. Hata hivyo Zari hakuwajibu chochote, bahati nzuri pia kwenye maoni ya ishu hiyo wapo pia mashabiki waliomuunga mkono mzazi mwenziye huyo na Mondi.
Toa comment