ZARI NA MADONGO YA GIZANI

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’

Mzazi mwenziye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amedaiwa kutupa madongo ya gizani kwa watu wanaomc-hokonoa kuhusu mpenzi mpya wa Diamond, Tanasha Donna.  

 

Kuna baadhi watu wamekuwa wakimsema mitandaoni kuwa ameachana na Diamond lakini bado anamuonea wivu kwa jinsi anavyojiachia na Tanasha.

Kwa kuonesha kwamba anawajibu, kwa siku za hivi karibuni, Zari ameonekana kuandika jumbe huku akitupia picha mbalimbali za ‘bata’ zake ambazo mashabiki wengi wa mrembo huyo wamezitafsiri kwamba anawajibu wale wanaomchimba kuhusu mpenzi wake wa zamani (Diamond) kuchukuliwa na Tanasha.

“Comment za wenye hasira ziwe fupi…. kwa nini maisha ya mtu yanakuumiza hivyo bana? Fanya yako…,” aliandika Zari katika moja ya posti zake Insta-gram

Toa comment