The House of Favourite Newspapers

ZARI: Nilikutana na Diamond ‘DM’

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’

HAKUNA ufalme unaodumu milele hapa duniani kwa sababu unaambiwa hata ile iliyokuwa ‘kapo’ matata Afrika Mashariki ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ bado hali ni tete.

Karibu mpenzi msomaji wa Gazeti la Ijumaa katika safu yetu hii mpya ya The First We Met (Tulivyokutana Siku Siku ya Kwanza) ambapo utawasikia wanandoa mbalimbali wakiwemo mastaa na wasiokuwa mastaa wakielezea namna walivyokutana na kuunda muungano wa kimapenzi. Hii itakupa uzoefu wewe msomaji juu ya namna watu wanavyokutana na kuyajenga maisha.

“Bado nakumbuka siku ya kwanza tulipokutana, kila mmoja alikuwa na aibu kumsemesha mwenzake,” hivyo ndivyo alivyoanza kusimulia Zari juu ya namna alivyokutana na Diamond kisha kufurahia maisha kabla ya hivi karibuni jahazi kwenda mrama.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini mwake, Uganda alikozaliwa mwanamama huyo yapata miaka 38 iliyopita, Zari alieleza kuhusu jinsi alivyokutana na baba huyo wa watoto wake wawili, Tiffah na Nillan.

Zari alifunguka kwamba, yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza na Diamond kupitia ukurasa wake na kumtumia ujumbe DM (Direct Messaging) kwenye Mtandao wa Instagram.

Zari alikiri jinsi ambavyo mapenzi kati yake na Diamond yalivyoanza baada ya kukutana ‘live’ kwenye ndege ambapo tulikuwa tunasafiri pamoja. “Nilizungumza naye kupitia DM, nilimwalika kuhudhuria kwenye sherehe yangu ya White Party nchini Uganda, lakini aliniambia kwamba nizungumze na meneja wake,” alisema Zari na kuongeza:

“Diamond alianza kunichunguza, baadaye tulibadilishana namba za simu na hapo ndipo uhusiano ulipoanza. “Tulikuwa tukipigiana simu kila wakati na kujikuta tayari ni wapenzi kabla ya kuwa mtu na mzazi mwenziye.”

 

Kuhusu kukutana kwao, naye Diamond alishakaririwa mara kadhaa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers akielezea namna ‘alivyomtokea’ Zari na kujiokotea dodo chini ya mpera ambapo walijikuta wakipendana kupita maelezo huku wakioneshana mahaba niue hadharani.

Kwa mujibu wa Diamond, baada ya kuwasiliana na mwanamama huyo kupitia DM, alikiri kukutana na Zari kwenye ndege wakati wanatokea Afrika Kusini kuelekea Bongo. Diamond alisema kuwa, baada ya kukutana na Zari ndipo akarusha ndoano live na kukubaliwa kiulaini kwa kuwa mwanamama huyo alishaonesha dalili za kuzimika.

Hata hvyo, hilo la kukubaliwa haraka lilipingwa na Zari ambaye alidai kwamba, ilichukua muda kukubali kuwa mpenzi wa msanii huyo. Zari alimalizia kwamba, pamoja na kumkazia, lakini hatimaye alijikuta akisema YES.

Baada ya kukubaliana wapenzi, Zari na Diamond waliingia kwenye uhusiano wa kupika na kupakua ambapo matokeo yake, walijaliwa watoto wawili kabla ya kuingia kwenye gogoro zito. Katika mgogoro wao wa kimapenzi, Zari alimtuhumu Diamond kumkosea heshima akimtuhumu kumsaliti waziwazi hadi kufikia hatua ya kuzaa na mwana-mitindo Hamisa Mobeto. 

MOBETO: NYUMBA TUNAYOISHI IMETOKA KWA DIAMOND – VIDEO

Comments are closed.